Tag: Babu Tale

Ujumbe Diamond kwa Babu Tale baada ya kushinda kura za Maoni

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa kampuni ya WCB, Diamond Platnumz ametoa ujumbe uliolenga kumpongeza Babu Tale ambaye pia ni meneja wake baada ya kushinda katika kura za maoni jimbo la Morogoro vijijini.
Msanii huyo ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ushindi alioupata Babu Tale ni wa kishindo na wao (pamoja na wasanii wenzake) wanasubiri tu kamati kuu imalize kisha waachie nyimbo za kampeni kwa ajili yake.