Mjengo wa Rihanna kama unavyoonekana kwa nje

Picha za ndani ya mjengo wa Rihanna

Advertisements

Moja ya ndoto ambazo watu wengi tunatamani kuwa nazo ni kumiliki Majengo makubwa na ya kifahari lakini zaidi ni kuishi maisha mazuri, hivi karibuni imeripotiwa kuwa nyota wa muziki nchini Marekani ambaye kwa sasa amejikita sana katika biashara pamoja na fashion hapa namzungumzia Rihanna Mkurugenzi wa kampuni za Fenty kuwa amenunua mjengo wa kifahari sana ulioko katika vilima vya Beverly huko Calfornia, Marekani.

Mjengo huo ambao kwa jina maarufu la ughaibuni unajulikana kama Beverly Hills Mansion umesheheni mabo kedekede ikiwemo vyumba vya vyoo 7, vyumba vya kulala 5, Jiko lililopambwa kwa Almasi, Bar iliyojazwa vinywaji, ukumbi wa kufanyia mazoezi na ukumbi wa kupumzikia ikiwemo na swimming pool ya kuogelea ambayo imepambwa taa zenye rangi za kuvutia mno.

Advertisements

Kama unvyojua jumba la msanii haliwezi kosa vifaa vyake vya kazi basi jumba hilo RiRi ameamua kuliwekea na ukumbi ambao ndani yake kumejazwa kila aina ya vifaa atakavyokuwa akivitumia kufanya muziki wake.

Zaidi na zaidi linalosumbua vichwa vya mashabiki wa Rihanna ni pale unapotazama pesa ambazo ameamua kuziwekeza katika kununua Mjengo huo Dola za Kimarekani Milioni 13.8 ambayo ni sawa na mabilioni ya Kitanzania.

Ikumbukwe kuwa historia ya mjengo huu ni kwmaba ulijengwa mwaka 1938, na Rihanna si Nyota wa kwanza kuishi ndani ya mjengo huu akiwa ameununua kutoka mikononi mwa Daniel Starr aliyekuwa mwanzilishi wa GameMime (source:Hollywoodlife) Hata hivyo kabla ya hapo mjengo huu ulikuwa ukikaliwa na binti wa Sidney Sheldon ambaye anajulikana kama Mary Sheldon.

Rihanna pia anamiliki majengo mengine ya kifahari kama ule ulioko katika jiji moja maarufu kama the century city ambao una gharama ya Dola Milioni 5.5 za Kimarekani, na mwingine unaopatikana katika vilima vya Hollywood ambao una thamani ya Dola 6.8 na amekuwa akiumiliki tangu mwaka 2019.