Baada ya mabingwa wa kike Tanzania Bara, Simba Queens kumtangaza Msanii nguli wa filamu za Bongo maarufu kama Monalisa kuwa msemaji wao. Monalisa mwenyewe ameandika waraka kupitia ukurasa wake wa instagram akieleza jinsi alivyofuarahia heshima aliyopewa na klabu hiyo.

Huku akiwa amepost na picha ambayo imemuonesha akiwa ameshikilia jezi ya Simba Queens ameandika kuwa anamshukuru mama Fetma Dewji kwa kumkabidhi kijiti cha kuwa msemaji wa Simba na kuahidi kuwa ataitangaza vyema klabu hiyo huku ushindi ukiwa mikononi mwao.

Hiki ndicho alichokisema monalisa baada ya kutangazwa kuwa msenaji wa Simba

Ukurasa wa instagram wa Monalisa