Shirika la Afya duniani limeonya kuwa kutokana na athari za kelele katika mazingira tunayoishi basi hadi kufikia mwaka 2050 huenda watu takribani Bilioni 2.5 watakabiliwa na changamoto kushindwa kusikia ipasavyo.

Mkuu wa shirika hilo Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa Jambo hilo linaweza kuleta madhira makubwa kwenye mawasiliano ya kila siku ya binadamu.

Advertisements

Taarifa hizo zimetolewa kwenye ripoti yake ya kwanza inayohusu hali ya kusikia ambapo imeandika kuwa endapo hatua stahiki hazitachukuliwa basi takribani watu Milioni 700 watahitaji huduma za kusikia au masikio kufanyiwa marekebisho.

Aidha WHO imekadiria kuwa watu takribani bilioni 1.1 wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 35 ndio walio kwenye hatari kubwa zaidi ya kupoteza uwezo wa kusikia.