CEO wa efm pamoja na tvetanzania almaarufu kama Majizo hivi leo amefunguka mazito kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost picha ya pamoja na mkewake na kuandika ujumbe ambao umeonekana amelenga kwa mashabiki zake pamoja na mkewe.

Majizo amefunguka nyakati ambazo mkewake amepitia ikiwemo matusi na kashfa za mitandaoni katika kipindi akiwa kwenye uchumba nae lakini pia amechukua nafasi hiyo kumshukuru mkewe Elizabeth kwa kuwa mvumilivu nyakati zote na kuwahusia vijana wengine ambao wapo kwenye mahusiano na wana ndoto za kufunga ndoa kuwa wavumilivu kwani safari bado ni ndefu sana.