Mwanamitindo na video vixen Jasinta Makwabe ambaye amedaiwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz amewajibu mashabiki ambao wamekuwa wakimtukana kutokana na kitendo cha kumpost na kumpongeza nguli huyo wa muziki katika ukurasa wake wa Instagram.

Akiwa anatoa maelezo ya jinsi ilivyokuwa Mwanamitindo huyo amesema kuwa kuna baadhi ya mashabiki wamemtumia ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram (DM) huku wengine wakituma jumbe za matusi wakimlaumu eti kwanini amempost Diamond Platnumz na kuwa huenda kufanya hivyo angeharibu brand yake kwani Diamond ni mtu mwenye scandals nyingi sana.

Akizungumza na Bongo5 amesema kuwa

“Nimegundua kuwa Watanzania ni rahisi sana kukutukana na kukukatisha tamaa ila hawapo tayari kukupongeza kwa kile kizuri unachofanya, mimi nimefanya vitu vingi sana ambavyo vilikuwa ni kuitangaza nchi ila sijawahi kupongezwa lakini baada ya kumpost Diamond nimetukanwa sana ..Why Diamond is a big deal ? kwanini sio wengine mbona huwa nawapost”

Yasinta Makwabe
Advertisements