BURUDANI

Masaa 36 ya mfungwa namba 8612- Doug Korpi

Wafungwa waliamua kuvunja mlango wa selo mojawapo na kutoka nje jambo ambalo liliwafanya maafisa wa polisi kutumia nguvu kuwarudisha ndani na hapo ndipo ukawa mwanzo wa vurugu zisizokuwa na ukomo.

Baada ya muda maafisa wa polisi walishauriana kutumia mbinu za kisaikolojia ili kuwatuliza wafungwa, waliamua kuchagua chumba ambacho walikiita selo ya upendeleo, na kuwaambia wafungwa wote kuwa kwa yule ambaye hatoleta vurugu basi aingie ndani ya chumba hicho na atapatiwa huduma nzuri zaidi.

Advertisements

Miongoni mwa wafungwa walioingia ndani ya seli hiyo ya upendeleo alikuwepo Mfungwa namba 8612, na baada ya kukaa muda mfupi ndani ya chumba hicho alianza kuonyesha mabadiliko.Unaambiwa ndani ya masa 36 Mfungwa huyu alianza kulia, kilio kisicho na ukomo, mawazo na hasira iliyopitiliza na aliporipotiwa kwa Profesa Philip Zimbardo pamoja na timu yake, walimpuuza wakidhani ni mbinu yake ya kutoroka ndani ya gereza.

Na ili kuonyesha kuwa jaribio lile lililenga ukweli, waliamua kumtisha Mfungwa huyo kumuambia kuwa endapo ataendelea kulia basi angepelekwa kwenye gereza lenye ulinzi wa hali ya juu zaidi, jambo ilo lilimtuliza mfungwa huyu kwa muda mfupi tu lakini baada ya dakika kadhaa hali yake iliendelea kuwa vilevile tena akilia kwa kuwaambia wenzake kuwa

“Huwezi kutoka, huwezi kughaili”

 Hali ya mfungwa namba 8612 ilizidi kuwa mbaya tena iliogofya sana kwa wafungwa wengine, alizidi kulia akisema kuwa anasikia maumivu na kuungua upande wa kichwani, hali hii ilizidi kuwa mbaya mno.

Baada ya kugundua kuwa ule haukuwa utani Zimabrdo na timu yake waliamua kumtoa mfungwa namba 8612 kwenye jaribio ilo, huku wakiwazuga wafungwa wengine kuwa kutokana na fujo alizoleta mfungwa mwenzao basi wameamua kuwahamisha na kumpeleka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi.

Na huo ndio ukawa mwisho mbaya wa Doug Korpi maarufu kama mfungwa namba 8612, miaka michache baadae wandishi wa habari mbalimbali walimtafuta Doug na kumuuliza jinsi alivyojisikia wakati alipokuwa ndani ya jaribio lile naye aliwajibu kuwa.

Anaamini kwamba hatua ambayo aliifikia kwake ilikuwa ni fake ili aweze kuachiwa huru kutokana na kuchoshwa na mateso ndani ya gereza, wakati huohuo Zimbardo yeye alijibu kuwa Doug alisema maneno hayo ya kujitetea kwani halikuwa hakumbuki kile kilichomkuta ndani ya gereza hilo.

Baada ya jaribio lile Doug Korpi aliamua kujikita kwenye masomo ya saikolojia na hivi sasa ni Profesa wa Saikolojia katika chauo kikuu cha Stanford huko Marekani.

SOURCES;

Pages: 1 2

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.