Mwezi Agosti mwaka 1971, Profesa na mtafiti wa masuala ya Kisaikolojia Phillip Zimbardo akishirikiana na Ofisi za Navy za USA aliandika Tangazo ambalo lilibandikwa kwenye kila kona ya mji wa Calfornia.

Tangazo hilo lilibeba maandishi yaliyowataka watu wenye akili timamu na afya njema kujitokeza ili kushiriki jaribio la kuchunguza athari za kisaikolojia zitokanazo na nguvu ya utawala wanayopewa Maafisa wa magereza kwa wafungwa.

Profesa Zimbardo na wenzake walitamani kuchunguza juu ya sababu ya uwepo wa tabia za kikatili wanazofanyiwa wafungwa na jinsi zinavyoathiri saikolojia zao. Tangazo liliandikwa kuwa jaribio lingefanyika kwa muda wa siku saba mfululizo huku kila mfungwa angelipwa kiasi cha dola 15 kwa siku, ambapo ni sawa na dola 90 (2017-) kwa miaka hii ya sasa.

Wengi walijitokeza ili kutafuta ridhiki kupitia jaribio hilo lakini wanaume 24 tu walipata nafasi ya kushiriki katika jaribio hilo na Bwana Doug Korpi akiwa mmoja wao.

Phillip Zimbardo akiwa na timu yake walianzisha jaribio hiyo kwa kuwagawanya wanaume hao 24 katika makundi mawili yaani wafungwa na maafisa wa gereza, kwa bahati mbaya Doug Korpi alijikuta amedondokea upande wa kuwa mfungwa.

Katika mavazi yake ilibandikwa namba 8612 na hapo ndipo ukawa mwanzo jina lake kubadilka, ili kufanya jaribio liwe ni kama maisha ya kweli basi waliochaguliwa kuwa maafisa magereza waliamrishwa kuwakamata wafungwa wao wakiwa mtaani na kuwapeleka kwenye gereza la kughushi lililoitwa Jordan Hall la Chuo kikuu cha Stanford.

Advertisements

Kama ujuavyo ni mara chache sana kukuta wafungwa wakila bata gerezani, vivyi hivyo kwa vijana waliodondokea upande huo, kila selo moja waliwekwa wafungwa watatu wakiwa wamebanana, huku maafisa wa polisi wakiwa wanakula upepo mwanana kwenye vyumba vyao.

Tena haikutosha! Maafisa hao walipewa majukumu ya kuwalinda wafungwa wale kwa kupokezana watatu watatu, kwa masaa nane na endapo utamaliza zamu yako basi ulikuwa ukiruhusiwa kurudi nyumbani.

Siku ya kwanza ya jaribio hilo ilienda vyema tena kwa utulivuu kabisa, lakini ilipokucha siku ya pili tayari wafungwa walishaanza kuchoka kukaa gerezani hivyo hapo kimbembe kikaanza.

Endelea kusoma ukurasa wa pili…..