Jumla ya majeneza 27 yaliyozikwa miaka 2,500 iliyopita yamefukuliwa na wanaikolojia nchini Misri.

Majeneza hayo yamefukuliwa kutoka kwenye makaburi yanayopatikana katika kisima kipya kilichogundulika eneo moja takatifu lililopo huko Saqqara kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Advertisements

Mapema mwezi huu yaligunduliwa majeneza 13 na sasa 14 zaidi yamepatikana, maafisa wanasema kuwa ugunduzi huo unasemwa na wataalamu kuwa ni ugunduzi mkubwa kuwahi kufanyika.

Majeneza hayo yamekutwa yakiwa na urembo wa rangi za kuvutia na kuhifadhiwa vitu vingine vidogo, Saqqara ni eneo ambalo wamezikwa wafu kwa zaidi ya miaka 3000 iliyopita.

Advertisements

Taarifa ya ugunduzi huo ilichelewa kutoka hadi Waziri wa mambo ya kale wa Misri, Khaled Al-anan alipotembelea eneo la ugunduzi na kujionea majeneza hayo yeye mwenyewe.

Waziri huyo aliwapongeza pia wanaikolojia waliyofanya kazi hiyo hadi kuikamilisha katika hali ngumu chini ya kisima cha urefu wa mita 11

Uchimbaji bado unaendelea kwenye eneo hilo huku wataalam wakijaribu kung’a mua nini kilikuwa chanzo cha makaburi hayo.