Advertisements

Ikiwa bado sakata la kufungiwa kwa mtandao wa Tik Tok linaendelea nchini Marekani hivi karibuni kumeibuka sakata jipya la kufungiwa mtandao mwingine wa Wechat ambapo utazuiliwa kupakuliwa kupitia ghala yoyote ile nchini Marekani.

Kuanzia siku ya Jumapili mitandao ya Wechat pamoja na Tik Tok itapigwa marufuku nchini humo endapo Donald Trump atatia saini ya kukubali kutekeleza mkataba wa mwisho idara ya biashara imesema itazuia watu kupakua programu hizo.

Utawala wa Donald Trump unasemakuwa kampuni zinazomiliki programu hizo ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani na inaelezwa kuwa huenda zikawasilisha maelezo ya watuamiaji kwa Chini, Japo kampuni husika pamoja na China zimepinga uvumi huo.

Advertisements

Wechat itafungwa siku ya Jumapili pia watu wanaweza kutumia Tik Tok mpaka siku ya tarehe 12 Novemba ambapo huenda ikafungwa endapo ushirikisho kati ya kampuni ya teknolojia ya Marekani iitwayo Oracle pamoja na kampuni mwenyeji wa Tik tok hautofikiwa muafaka.

Advertisements

TIK TOK NI NINI?

Ni programu ambayo humuwezesha mtumiaji kupakia video ya sekunde 15 ambayo mara nyingi hujumuisha nyimbo fulani kama vile za wasanii aua wachekeshaji mbalimbali.

Vijana walio chini ya miaka 20 ndio wanaokadiriwa kutumia kwa wingi mtandao huo huku wakionyesha vibwanga vyao kwa wafuasi wao.

Inasemekana kuwa programu hii ina wafuasi karibia milioni 800 na wengi wao ni kutoka Marekani na India.