Advertisements

View Survey

Kupitia ukurasa wake wa Instagram rapper Cardi B ameweka wazi sababu ambazo zimemfanya kuhitaji kukatisha mahusiano yake ya kimapenzi na baba wa watoto wake Offset ikiwa ni baada ya miaka mitatu ya kuishi nae katika ndoa.

Rapper huyo ambaye anatamba kwa wimbo wake wa WAP alioutoa hivi karibuni amesema kuwa “hamna chochote kilichotokea ambacho kimesababisha yeye kutengana na mumewe” kupitia Insta live yake siku ya Sept 18 Cardi B aliwahakikishia mashabiki zake kuwa yuko salama na hatomwaga machozi tena kama ilivyokuwa mwanzo. (Scandal ya Offsset kutoka nje ya ndoa yao)

Advertisements

Cardi B ameongeza kwa kusema kuwa maamuzi yake ya kuvunja ndoa yao na Offset hayahusiani na maigizo ya kimapenzi yanayoendelea midomoni mwa watu kwamba Offset anatoka nje ya ndoa au ana mtoto wa nje jambo ambalo kwake yeye (Cardi B) haoni kama ni kweli.

Video from Hollywoodlife.com

Lakini pia Cardi B akaendelea kwa kusema kuwa sababu ambayo imemfanya akatishe mahusiano yao ni amechoshwa kuhusishwa na kugombana juu ya uvumi unaoendelea kuhusu Offset pia amechoshwa na kutoshuhudia mambo yanayoendelea kwa macho yake mwenyewe “unapohisi mambo hayaendi sawa kama ilivyokuwa mwanzo ni vizuri ukaachana nayoo tu” alisema Cardi B.

View Survey

Advertisements