Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani, Rihanna amewatoa hofu mashabiki zake baada ya kuwaambia kuwa wasione yuko kimya wakahisi ameacha kufanya muziki bali anaandaa muziki mzuri kwa ajili yao
Mwanadada huyo aliyetamba kwa ngoma ya ‘Work’ hakuwahi kutoa albamu nyingine yoyote tangualipoachia albamu yake ya mwisho iliyoenda kwa jina la ‘ANTI’ mwaka 2016, hivi karibuni amesema kuwa anaifanyia kazi albamu ijayo mpaka atakapokuwa amejiridhisha ndipo ataiachia mtaani.
- Babalevo atangaza vita kwa yeyote atakayemtukana Diamond
- Masaa 36 ya mfungwa namba 8612- Doug Korpi
- Samatta ajiunga na Fenerbahce, Aston Villa FC yashuka followers
- Tanzania: Panya anayeweza kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini, atuzwa
- Swizz Beatz afunguka sababu za Diamond kuimba Kiduchu kwenye Wasted Energy

Ukitupilia mbali muziki anaojihusisha mwanadada huyo bado amejikita kwenye biashara za vipodozi vilivyobebwa na ukubwa wa jina lake ‘Fenty Beauty’ Hivi karibuni sauti ya Rihanna iliweza kusikika kwenye ngoma aliyokuwa ameshirikishwa na Partynextdoor ilyokwenda kwa jina la ‘Believe it’
Rihanna ashirikishwa katika nyimbo mpya ya PARTYNEXTDOOR “Believe it”
Categories: BURUDANI