Facebook imesema kuwa itamzuia mgonjwa wa maradhi yasiyo na tiba kurusha video mubashara za kifo chake kupitia mtandao huo wa kijamii.
Alain Cocq mgonjwa mgonjwa mwenye umri wa miaka 57 alipanga kurusha video zinazooneshs maisha yake ya siku za mwisho kupitia mtandao wa facebook baada ya kuanza kukataa chakula na kumeza dawa kuanzia siku ya jumamosi.
- Ben Pol kudai talaka kwa mkewe kulikoni?
- Kim Kardashian atabiri bilionea atakayefuata
- Nyuma ya pazia,Satan ya Rosa Ree|Rosa afungukia mahusiano yake
- Alilolisema Makonda wakati wa mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
- Download audio| Tanzania All Stars- Lala salama
Bwana Cocq aliomba sheria ya Ufaransa ibadilishwe na iruhusu mtu kuondolewa uhai wake kama watakavyopenda pale anapokuwa kwenye maumivu makali lakini baadhi ya makundi kama Kanisa la Katholiki wamepinga ombi lake.
Rais wa Ufaransa Emmanuela Macron pia ni mmoja kati ya waliotupilia mbali ombi hilo.

“Njia ya ukombozi inaanza na niamini nina furaha” Bwana Cocq aliweka maneno hayo kwenye mtandao wa Facebook akiwa nyumbani kwake mjini Djon siku ya jumamosi.
“Najua siku kadhaa zitakuwa ngumu mbeleni lakini nimefanya uamuzi na niko utulivu” aliongeza
Bwana Cocq anasumbuliwa na ugonjwa ambao umeathiri tishu na viungo na kusababisha kuta za mishipa ya ateri kushikana
Lakini Facebook imezuia mpango wake huo ikisema kuwa hairuhusu kurusha matukio ya kujitoa uhai kurushwa kupitia mtandao huo
“ingawa tunaheshimu uamuzi wa Bwana Cocq kutokana na ushauri wa kitaalamu tumechukua hatua kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya suala la Alain” Msemaji wa Facebook ameliambia shirika la habari nchini humo AFP.