Mchekeshaji na mwigizaji maarufu nchini Marekani Whoopi Goldberg amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni baada ya kuziomba studio za kutengeneza filamu za Disneyland na DisneyWorld kujenga hifadhi ya Wakanda kama sehemu ya kutoa heshima kwa Chadwick Boseman.

Advertisements

Tangu kutokea kwa kifo cha muigizaji maarufu duniani Chadwick Boseman ambaye ndiye aliyeigiza kama Mfalme wa kabila la kubuni la Wakanda kwenye filamu ya Black Panther, watu wengi maarufu wametoa heshima zao kwa kwa marehemu Chadwick.

Advertisements

Ikiwemo studio za Disneyland, Marvel pamoja na Avengers, hivi karibuni mchekeshaji kutoka nchini Marekani Whoopi ametoa ombi kupitia ukurasa wake wa twitter kwenda kwa studio Disneyland na DisneyWorld kuwa ni vyema kama wakitengeneza sehemu ambayoitakuwa kama hifadhi ya Wakanda kutoka katika moja ya Hifadhi za Studio hizo.