Hollywood yote ipo katika majonzi hivi sasa baada ya kumpoteza moja kati ya waigizaji nyota na mashuhuri Chadwick Boseman ambaye amefariki Agosti 28 kwa ugonjwa wa kansa ya utumbo mpana.

Nyota huyo ambaye amejulikana kwa jina la T’challa ambalo ndilo aliloigizia kwenye filamu ya Black Panther, familia yake imethibisha kuwa Chadwick amepitia katika vita ya kupambana na kansa kwa muda wa miaka minne kabla ya kufariki kwake “ni kwa huzuni isiyopimika tunathibitisha kifo cha Chadwick Boseman”.

Hapa tumekuletea mambo 5 ambayo huenda hukufahamu kuhusu T’challa na taaluma yake ya uigizaji pamoja na maisha ya nje na uigizaji.

  • Vita yake ya siri dhidi ya kansa inahusishwa na tabia yake ya kuweka mambo yake faragha;

Ingawa T’challa amekuwa muigizaji kwa muda usiopungua muongo mmoja bado alijaribu kuweka maisha yake binafsi kama faragha, hakuna aliyeweza kutambua mambo mengi aliyokuwa akiyapitia kama vile scandals za mahusiano, kama vile ilivyokuwa kwa mastaa wengi.

Advertisements

Siku moja kwenye mahojiano aliulizwa kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi alijibu kuwa hii siyo biashara ya mtu mwingine yoyote ila mimi, wengi wenu munanifahamu kama Chadwick muigizaji, na inatosha mukinitambua hivyo tu.

  • Chadwick alikuwa na familia kubwa sana.

Chadwick aliwahi kusema kwenye mahojiano yaliyofanywa baina yake na Mr Porter kuwa bibi yake alipofariki aliacha wajukuu na vitukuu 115.

Advertisements
  • Taaluma yake ya uigizaji ilianza kwenye Runinga.

Mara nyingi waigizaji wakubwa wengi huwa wamepitia katika uigizaji wa tamthilia ama michezo ya kawaida inayoonyeshwa kwenye runinga, vivyo hivyo kwa Chadwick kabla ya kuwa maarufu kama T’challa nyota wa Black Panther na Avemger alianza kuwa muigizaji wa runinga kwenye filamu iliyorushwa kwa jina la Law and Order CSI. ER, Castle, Fridge na nyingine nyingi

Advertisements
  • Alikuwa akipenda kushiriki michezo akiwa shule,

Waigizaji wengi huwa wanapenda kushiriki michezo hasa mchezo aina ya mpira wa kikapu, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa T’challa enzi za uhai wake, alikuwa ni mtu aliyependa kushiriki michezo “nilicheza ligi ndogo ya mpira wa kikapu” alisema muigizaji huyo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na jarida la Vanity Fair

  • Hakutakiwa kuingiza sauti kwenye filamu ya Black Panther

Baada ya rais wa studio za Marvel Kevin Feige kuona uigizaji wa Chadwick kupitia filamu ya Get On Up ndipo sasa Kevin alitambua kuwa Chadwick angekuwa mtu sahihi kuigiza kama Mfalme T’challa.

“nafikiri ilikuwa kama jambo la masaa 24 baada ya kulitaja jina lake kwenye kika cha utengenezaji wa hadithi ya filamu na kuongea na mawakala wake na kisha kumpigia simu na kumuomba aigize kama Mfalme T’challa kwenye Black Panther naye alikubali” alisema Kevin

Advertisements