Advertisements

Picha ya Simba katika nembo ya Ligi kuu nchini Uingereza inaweza kuwa si maarufu sana miongoni mwa mashabiki wa mpira licha ya umaarufu wa ligi hiyo kubwa na pendwa duniani.

Hii ni kutokana na kutoifahamu historia na maendeleo ya mpira nchini humo, leo nakuletea mwanzo mwisho kisa na mkasa cha umaarufu wa nembo na ligi hiyo pendwa duniani.

Historia ya mpira wa Kiingireza imetoka mbali sana, licha ya timu zake kuwa na mafanikio lukuki kwenye mashindano ya ulaya mwanzo wa ligi hiyo ulianzia miaka ya 80.

Kabla ya miaka hiyo ya 80 viwanja vingi nchini humo vilitelekezwa hivyo kufanya mashabiki nchini humo kuuchukia mpira hata kupelekea timu nyingi kukosa sifa za kushiriki mashindano ya ulaya.

Advertisements

Hali haikuwa shwari ligi hiyo ikaanza kupoteza wachezaji wengi wenye vipaji, sasa basi serikali ya nchi hiyo ikaamua kufanya mabadiliko kadhaa wa kadhaa ili kufanya mchezo huo pendwa dunia kuendeshwa kibiashara zaidi, viwanja vilijengwa upya hii ikafanya wadhamini mbalimbali kuvutiwa kuwekeza kwenye ligi hiyo.

Uwekezaji ukaifanya ligi hiyo kuwa ya kibiashara kuanzia miaka ya 90 hasa baada ya mfumo mpya wa undeshaji ulipobadilika mwaka 1992 na huu ndo ukawa mwanzo wa maendeleo ya nembo ya Ligi kuu nchini Uingereza.

Advertisements

Nembo yenye mwonekano wa Simba mkubwa ilichakuguliwa kama ishara ya maendeleo ya mpira wa nchi hiyo duniani tangu mwaka 1872.

Picha ikionyesha mabadiliko ya nembo ya Ligi kuu nchini Uingereza tangu mwaka 1992. Picha na mtandao

Waingireza hadi leo wanaamini ligi yao ina nguvu kuliko ligi zote duniani ndio mana wakachagua nembo ya Simba ambaye mwituni hujulikana kama mfalme wa wanyama wote hiyo nembo yao katika mwonekano huo itamaanisha hivyo siku zote kizazi na kizazi.