Madam Rita afunguka kuhusiana na wimbo wa msanii wa bongo fleva na Mkurugenzi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize, ambao umekuwa na maudhui ambayo yamezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Advertisements

Kama umefanikiwa kuitazama nyimbo ya JESHI iliyoachiwa hivi karibuni na mwanamuziki Hamonize kutoka Konde Gang naamini utakubaliana na mimi kuwa kuna kipande cha video ambacho kimemuonesha Harmonize akikataliwa kwenye mashindano ya BSS.

Advertisements

Boss wa mashindano ya BSS Madam Rita amefunguka hivi leo kupitia EATV na EA Radio Digital akizungumzia sakata zima jinsi lilivyoanza mpaka hapo lilipofikia, Pia Madam Rita ameweka wazi kuwa hawana tatizo lolote na Harmonize

“Hatuna tatizo naye ni msanii mzuri ila kwa kipindi kile alivyopita alikuwa bado hajajiandaa vizuri sio kwamba tulimchukulia poa na tulikuwa hatumfahamu na ni mambo ya kawaida tu, tunamkubali jinsi anavyong’aa kwa sababu alipita pale, sekunde 30 huwezi ukaona kipaji cha mtu ila baad ya muda unaweza ukaona” amesema Madam Rita.

Chanzo: EATV na EA Radio Digital