Msanii wa Bongo Fleva Shetta ameweka wazi historia iliyopo kati yake na binamu aka Mwana FA kwa muda wa miaka kumi.

Shetta ameandika ujumbe mrefu sana kupitia ukurasa wake wa instagram uliosomeka “Watu wengi Hawajui kuwa Binamu yetu Hamis Mwijuma Ndo msanii wa Kwanza kabisa Kufanya nae wimbo wangu wa kwanza kunitambulisha kwenye Mziki miaka 9 iliyopita Ikiwa ni msanii Mchanga, Wimbo huo unaitwa, #Menaplay.
hakuna anaenijua kwenye tasnia hii”
ameandika Shetta

Latest Posts

Advertisements

“Ikiwa baada ya kuhangaika sana kutafuta mtu ambae atanisaidia sauti yake kwenye wimbo wangu kipindi kile, Too bad kuna wasanii wakubwa tu walikuwepo na wengine wametangulia mbele ya Haki (RIP) walikataa wengine walitaka niwalipe tena niwalipe Hela nyingi na sikua na pesa yoyote kipindi kile. But @mwanafa Alinipa muda wa kunisikiliza na mtihani pekee alionipa ni kwamba kama wimbo utakua mkali sana atafanya na mimi. Kama utakua mbaya basi tuendele kuwa mtu na mdogo wake tu hatofanya. Lol” ameongeza Shetta

Post ya Shetta IG
Advertisements

“Na baada ya Kusikiliza wimbo huo moja kwa moja alikuja studio na akaingiza sauti, na Hata baada ya kumaliza nikataka kumpa hela kidogo ya Usumbufu japo ya Mafuta akakataa. Kiukweli MwanaFa ni Mtu na Nusu. Nimejifunza mengi na naendelea kujifunza kutoka kwako vitu vingi. Kiukweli Nakukubali sana… Sasa inabidi itoke Nyingine kali baada ya Miaka 9 iliyopita” mwisho wa kunukuu.

Advertisements
Advertisements