Muandaaji wa mashindano ya Bongo Star Search BSS Madam Rita ameomba radhi mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kwa kuchelewesha malipo ya aliyekuwa mshindi wa mashindano ya BSS Meshack Fukuta, msimu uliopita mwaka 2019.
Trending Stori
- Ben Pol kudai talaka kwa mkewe kulikoni?
- Kim Kardashian atabiri bilionea atakayefuata
- Nyuma ya pazia,Satan ya Rosa Ree|Rosa afungukia mahusiano yake
- Alilolisema Makonda wakati wa mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
- Download audio| Tanzania All Stars- Lala salama
Muaandaji huyo ameyasema hayo akiwa kwenye hafra fupi ya uzinduzi wa mashindano ya BSS msimu wa 11, huku Meshack akiwa mmoja kati ya watumbuizaji kwenye uzinduzi huo.
Aidha Madam Rita ametangaza kauli mbiu ya BSS mwaka huu ambayo ni “mpya kubwa na nusu”

“pia nichukue fursa hii kuomba radhi watazamaji wetu, washiriki wetu na wafuatiliaji wa Bongo star search kwa sintofahamu iliyotokea mwaka jana kwa kucheleweshwa kwa malipo ya mshindi wa Bongo star search Meshack Fukuta tunaomba radhi sana ni changamoto iliyotokea,na uhakika mulikwadhika hivyo niombe radhi kwani ni matatizo yaliyokuwepo nje ya uwezo wetu nasi tunawaahidi hii haitojirudia tena” amezungumza Madam Rita