Msichana mwenye umri wa miaka 15, picha yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha ameshika bunduki aina ya AK 47 ya baba yake aliyoitumia kutetea familia yake kwa kuua wanaume wawili na kumjeruhi watatu wakati walipovamia nyumbani kwao.

Advertisements

Majina yaliyotumika yamebadilishwa kwasababu za kiusalama

Nooria msichana kutoka nchini Afghanstan ameibuka shujaa baada ya kutumia bunduki na ujuzi alioupata kutoka kwa baba yake jinsi ya kutumia bunduki na baadae kuitumia kusaidia familia yake ilipovamiwa na waasi wa Taliban.

Akizungumza na BBC Nooria amesema kuwa wanaume hao waliwasili kijijini kwao ikiwa ni usiku wa manane na kuingia kwenye nyumba yao kupitia mlango wa mbele na kisha kuwachukua wazazi wake na kuwatoa nje ya nyumba.

Anaeleza kuwa baada ya kuwatoa waliwapeleka nyumba ya mbele eneo la milimani na baada ya hapo alisikia mlio wa risasi. “waliwaua”

Baada ya kusikia mlio wa risasi Nooria hakuwa na uwoga wa kujificha tena aliinuka na kuchukua bunduki aina ya AK-47 na kutoka nje kisha kufyatulia risasi wanaume hao waliokuwa nje ya nyumba yao.

‘Amesema alifyatua risasi mpaka akakaribia kuzimaliza zote’

Advertisements

Baada ya saa moja kukawa kimya hali iliyoonyesha kuwa wanaume hao wamesaimu amri, mahala pa tukio palikuwa na miili tano wa mama na baba yake wa jirani yao pamoja na wanaume wawili.

“Hali ilikuwa inatisha sana, baba yangu alikuwa mlemavu na mama yangu hakuwa amefanya lolote lakini waliwaua bila sababu” alisema Nooria

Nooria anaongeza kuwa kuzaliwa na kuuklia Afghan, watoto na vijana kama yeye huwa hawajui kingine zaidi ya Vita tu mgogoro unaoendelea kati ya wanamgambo wanaopendelea vikosi vya Taliban umekuwepo kwa takribani miaka 25.

Vikosi vinavyopendelea serikali vinadhibiti miji mikubwa huku huku Taliban wakijtwalia maeneo ya vijiji.

Hata hivyo kundi la wanamgambo wa Taliban limekanusha kuhusika na shambulizi hilo, huku wakiafiki kuwepo kwa shambulio katika kijiji hiko usiku ule na kusema kuwa kituo cha wanamgambo wa Taliban kililengwa na Polisi kisha kusababisha majeraha kwa wanaume wawili wa Taliban.

Advertisements
Nooria na kaka yake wakiingia kwenye helikopta

Source BBC

For you to listen to good African music visit >>> AFRICAN MUSIC