Afisa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara ameeleza kuwepo kwa wiki ya Simba ambayo itaitwa Champions Week au Wiki ya Mabingwa inayoanza hivi leo tarehe 14 Agosti na kufikiwa kilele chake siku ya tarehe 22 Agosti.

Advertisements

Manara amefunguka kuwa wiki hii itaambatana na uzinduzi wa jezi mpya za Simba watakazozitumia msimu ujao 2020/21, pia uzinduzi wa logo mpya ya klabu ya Simba pamoja na kutambulisha wachezaji wapya.

Download mp3 Audio: Navy Kenzo ft Tiggs Da Author – Pon Me

Kauli mbiu ya wiki ya mambingwa ni Simba Another Level

Aidha Manara ametupa jiwe gizani kufuatiwa na msemo wake “Wiki hii Mabingwa wanajinafasi tunaomba Watanzania wengine watuachie wiki yetu tunalo jambo letu