Advertisements

Giza limeanza kupotea na ndege wanalia kuashiria kwamba ni asubuhi na mapema sana katika ngome ya Makhuwa, Kusini mwa bara la Afrika. Baragumu limesikika na watu wameamka kukimbilia nyumbani kwa chifu Soshangane, kujua kulikoni. Mbona anawaita mapema hivi?

Kisa cha asubuhi hii ni kuzaliwa kwa mtoto wa ajabu ambaye wazazi wake wanaamua kumwita Luis Miquissone ambaye hakuwa anajulikana kama atakuja kuwa na kipaji cha soka kwenye miguu yake ya dhahabu.

Advertisements

Pasi na shaka hakuna mtu asiyeujua uwezo wa Miquissone awapo uwanjani kwani unaweza ukamfananisha na Lionel Messi kwa namna anavyojua kuuchezea mpira.

Basi kisa hiki alikuwa nacho mganga mmoja mashuhuri sana ndani ya ngome ya watu wa Khoisani. Mbele ya chifu na watawala wote mganga Manjakazi amepiga magoti anaomba ridhaa ya kuwasilisha maono aliyoyapatiwa na miungu wa ufalme usiku wa jana.

Kwa mkwara na midadi mingi Manjakazi anasema, “miungu wameukumbuka ufalme wetu. Wamesema wamesikia sala zetu na baada ya mavuno yajayo atazaliwa mtoto mmoja wa ajabu. Atafanya kazi zote za ufalme bila kuchoka. Atalima mashamba yetu yote peke yake. Ataweza kupigana na wanajeshi elfu tisa peke yake. Atakuwa na nguvu za ajabu sana. Hivyo, hatutahitaji kufanya kazi tena.

Basi kwa furaha kubwa chifu anaagiza siku hiyo ifanyike sherehe, watu wanywe pombe kuwafurahia miungu. Ila miaka ilipita na yule mtoto hakuzaliwa. Badala ya furaha yalikuja majanga. Chifu Soshangane akafariki.

Wakaja waarabu wakawauza utumwani, jina la ngome likabadilishwa kuwa Msumbiji, wakaja Wareno wakawatawala. Badala ya furaha ilikuja huzuni. Mpaka leo watu wa msumbiji wanamsubiri yule mtoto wa ajabu azaliwe ili awaletee furaha.

Advertisements

Nimekisoma hiki kisa, kisha nikamfikiria tena Luis Miquissone, nikajiaminisha huyu ndiye yule mtoto wa ajabu waliokuwa wanamsubiri. Labda yule mganga alitumia tu fasihi kuwaficha watu. Labda, Huwezi kujua. Fikiria, mpira wote ule alionao ‘Miqu’ anakuwaje muafrika? anakuwaje mmozambique? Anachezaje simba?

Alifika Mamelodi Sundowns mapema sana akiwa na miaka 19 tu. Ila waliamini bado ni mtoto. Wakamzururisha kwa mkopo. Mpaka Simba walipomtaka. Mara zote umuonapo uwanjani, utamuona na ‘miguu ya kibrazil.’ Atapiga chenga, atatoa pasi, atapiga krosi na atafunga. Atakufanya uone mpira ni mchezo rahisi sana. Wala hana mbwembwe, yeye kazi tu.

Advertisements

Mtazameni sana Miqu, Kisa tu amevaa jezi ya Mussa Hassan ‘Mgosi’ basi kaa ukijua anatudanganya kuwa uwezo wake ni wa kucheza hapa kwetu.