Msanii wa muziki wa Bongo flava, Shetta amefunguka na kusema kuwa wanawake si viumbe dhaifu kwasababu amebahatika kuingia leba na kuona jinsi mkewe mama Qayla alivyojifungua kwa uchungu.

Shetta amesema kuwa wanawake ni watu ambao wanatakiwa kuheshimiwa sana kutokana kitendo cha kutunza ujauzito tumboni kwa miezi 9 na kumleta duniani ni kazi ngumu ambayo ni sawa na nusu kifo

Advertisements
Msanii Shetta

“Nilimuona mkewangu Mama Qaylah wakati anajifungua mtoto wetu wa pili, nafikiri wanawake ni watu ambao tunatakiwa tuwaheshimu sana kwasababu kitendo cha kubeba ujauzio miezi 9, ile hali ya kujifungua inakuwaga nusu kifo na kazi kubwa ni kitendo cha kulea watoto sipendi kabisa mtu anasema mwanamke ni kiumbe dhaifu” amesema Shetta

Chanzo EATV.TV