Mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Marekani Kylie Jenner ameweka wazi kuwa hakuna tofauti kati yake na dada yake Kim Kardashian kufuatiwa na kuwepo kwa uvumi unaoendelea kuwa wawili hao wapo kwenye mgogoro.

Akizungumza kwenye Keeping up with Kardashians, Kylie Jenner amesema kuwa licha ya makampuni yao ya biashara za urembo na vipodozi yapo tofauti, haimaanishi kuwa hata wao pia wapo tofauti.

Advertisements

Pia Jenner ametoa sifa kwa dada yake na kampuni yake ya KKW Beauty alipokuwa akiongelea jinsi wanavyosaidiana katika kupeana ushauri kuhusu biashara pamoja.

TRENDING STORI

“Kim anaweza kutumia urembo wangu nami nikatumia wake, lakiini linapokuja suala la kampuni hapo ndipo tunapoachana, -japo bado tunakuwa pamoja katika kupeana ushauri” amesema Kylie.

Kim Kardashian na Kylie Jenner
Kim Kardashian kulia, Kylie Jenner kushoto picha na Hollywoodlife.com
Advertisements

Kylie pia amezungumza kuhusu familia yao, ushirikiano wao na dada zake wengine ambao ni Kourtney Kardashian 41, Khloe Kardashian 36, Rob Kardashian 33, na Kendall Jenner 24, amefunguka kuwa bado wana upendo katikati yao na wote hukumbushana juu ya baraka walizonazo

Advertisements
Kim Kardashian Photo by David Fisher
Advertisements
Kim Kardashian West Photo by Stephen Lovekin