Advertisements

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliono klabu ya Simba Haji Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ujumbe kuhusu uvumi unaoenezwa kuwa kiungo wao Clatous Chota Chama amejiunga na klabu ya Yanga.

Manara ameandika hivi; “Tetesi za Chama kwenda kucheza utopolo msimu unaokuja ni upumbavu, Chama ana mkataba na machampioni wa nchi hii hadi July 2021, Simba haiwezi kumuuza ama kumuachia mchezaji ambaye tuna malengo naye waacheni mazuzu fc waendelee kujidanganya najua viongozi wao wanataka kuwaongopea watu ili kutoa droo na ishu ya Morrisson, Chama wao ni yulealiyeenda jana”

Advertisements