Advertisements

Baada ya klabu ya Juventus kutangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu Maurizio Sarri , mabingwa hao wa Italia hatimaye wamemtangaza Andrea Pirlo kuchukua mikoba yake kwa mkataba wa miaka miwili.

Maamuzi hayo yamekuja ikiwa imepita siku moja tangu klabu hiyo iondolewe na Olympique Lyon katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya siku ya ijumaa usiku.

Advertisements

Pirlo ambaye aliwahi kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo kati ya mwaka 2011 hadi 2015 katika michezo 165 aliyoicheza, amechaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ya Italia ikiwa ni siku 10 tu zimepita tangu apate kazi ya kufundisha kikosi cha chini ya umri wa miaka 23.

Taarifa kutoka ndani za klabu iliyotolewa mapema jana ilisomeka , “Klabu imeamua kumwamini kwa kumpa kazii pamoja na benchi lake la ufundi kwani tzari alishakuwa kocha wa kikosi cha umri chini za miaka 23, pia yeye ni mtu anayejua nini kifanyike kuongoza hivyo matumaini yetu atatupeleka kwenye mafanikio”.

Advertisements

Vyanzo vingine vimeripoti kukosekana kwa maelewano baina yake na Cristiano Ronaldo kwa siku za hivi karibuni pia ndio sababu ya kufutwa kazi na miamba hiyo ya Italia.