MICHEZO

Wachezaji Simba wang’ara usiku wa tuzo VPL

Advertisements

Tuzo mbalimbali za wachezaji na vilabu zimetolewa usiku huu huku wachezaji kadhaa kutoka Simba wameonekana kungara kwenye utoaji wa zawadi mbalimbali zilizotolewa katika hafla lliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Wachezaji kadhaa kutoka Simba wamengara zaidi katika tuzo hizo hasa mchezaji Clatous Chama aliyejinyakulia zawadi ya mchezaji na kiungo bora wa msimu huu.

Clatous Chama mshindi wa tuzo za mchezaji na kiungo bora wa msimu. Picha na Instagram
Advertisements

Wengine kutoka klabu hiyo ni Meddie Kagere ambaye amenyakua ya ufungaji bora pia kwa upande wa tuzo ya kipa bora wa msimu nayo imetua msimbazi kwa Aishi Manula.

Mbali na wachezaji hao wengine waliondoka na tuzo ni Novatus Dismas kutoka biashara ambaye amepata ya mchezaji Chipukizi, Nicolaus Wadada beki bora pamoja na Paston Shikala bao bora kutoka Mbeya City.

Advertisements

Kwa upande mwingine kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck raia wa Ubeligiji amepata tuzo ya kocha bora wa msimu huku Kagera Sugar ikipata zawadi ya kuwa timu yenye nidhamu bora msimu huu.

Tuzo hizi ni za kwanza tangu kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania irejee tena kudhamini ligi kuu msimu huu.

Categories: MICHEZO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.