Advertisements

Mchezo wa hisani kati ya timu Samatta na Alikiba alimaarufu kama ‘Nifuate’ hapatoshi unaambiwa kwani tayari tambo zinaendelea kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho (leo) jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Wakitoa tambo zao kwa nyakati tofauti mbele ya waandishi wa habari Samatta na Kiba kila mmoja ametamba kumfunga mwenzake katika mchezo huo wa kesho (leo).

“Mwaka huu mimi na timu yangu tumejipanga vizuri kuchomoza na ushindi katika mchezo huo wa kesho mana nina kikosi kipana”. Alisema Kiba

Mbwana Samatta kushoto na Ali Kiba katikati kwenye mkutano na waandishi wa habari. Picha na Instagram
Advertisements

Kwa upande wa Mbwana Samatta alisema kuwa hana sababu ya kumuhofia Ali Kiba kwani michezo miwili iliyopita alichomoza na ushindi hivyo anaamini atashinda mchezo huo.

“Kwanza namshukuru Mungu nimerejea nyumbani salama, pia niwashukuru wadau wote wa michezo kwa sapoti yenu. Kuelekea mchezo wa kesho (leo) dhidi ya timu Kiba naahidi ushindi mana rekodi inanibeba mimi ukizingatia michezo miwili iliyopita nilishinda hivyo sina sababu ya kumuhofia Ali Kiba”. Alitamba Samatta

Advertisements

Mbali na tambo hizo unaambiwa mwaka huu ni balaa kwani timu Samatta yupo Clatous Chama ‘Mwamba wa Lusaka’ huku kule kwa Kiba yupo Bernard Morrison mzee wa kuupanda mpira hivyo kuufanya mchezo huo kuwa na hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka nchini.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na kuvutia licha ya maandalizi yake kuchelewa, hii itakuwa ni mara za tatu kufanyika, huku timu Samatta ikishikilia rekodi ya kushinda michezo miwili ya mwisho hivyo kufanya mechi hiyo ya le kuwa ya kisasi zaidi.