Advertisements

Azam FC imekamilisha usajili wa golikipa wa kimataifa wa Tanzania, David Mapigano Kissu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya

Kissu ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC.

Kipa huyo aliyechezea timu za Njombe Mji na Singida United, kabla ya kutimkia nchini Kenya amekuwa na msimu nzuri akiwa na Gor Mahia, takwimu zikionyesha amecheza jumla ya mechi 15, akiwa hajaruhusu wavu wake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo.

Pichani ni kipa mpya wa Azam Fc David Kissu akitambulishwa baada ya kusaini mkataba miaka miwili. Picha na Instagram
Advertisements

Nyota huyo aliyekuwa kipa namba moja wa Gor Mahia, pia aliweka rekodi ya kufunga bao, akifunga kwa mpira mrefu wa moja kwa moja, wakati Gor Mahia ikiilaza Bandari mabao 3-0.

Advertisements

Huo ni usajili wa tano kwenye kikosi cha Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, wengine waliosajiliwa wakiwa ni Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ayoub Lyanga na Ismail Aziz Kada.