Advertisements

Msanii wa mziki wa Bongo fleva Nchini Tanzania, Kharid Muhamedi (TID) amekilalamikia Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutumia msemo au ushairi wake wa “Ni yeye” katika shughuli za kisiasa bila lidhaa ya msanii huyo.

Advertisements

Tid amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amesikitishwa na kitendo hicho kilichofanywa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA

“Nimeona kwenye mitandao ya kijamii ushairi wangu ,ubunifu wangu ,msemo wangu kutumika katika kampeni za kisiasa pasipo kuwa na maelewano”

Advertisements

Ni yeye , Ni msemo ambao wanachama wengi wa CHADEMA wamekuwa wakiutumia katika kampeni zao huku wakimtaja Lissu kwa kutumia msemo huo.

Advertisements