Advertisements

Licha ya kuwa kinara wa mabao na fundi wa kufumania nyavu ligi kuu Tanzania Bara, mshambuliaji wa Simba Medie Kagere, ameachwa na kamati ya Tuzo Vpl baada ya kamati hiyo kutoa majina ya wachezaji watakao wania tuzo ya Mchezaji Bora.

Kagere ndiye mchezaji mwenye magoli mengi kuliko mchezaji yoyote VPL , amemaliza msimu wa 2019/2020 akiwa na jumla ya magoli 22

Advertisements

kamati ya Tuzo ligi kuu Tanzania Bara baada ya kutoa majina ya wachezaji watakaowania tuzo ya Mchezaji Bora, jina la mshambuliaji huyo halikutajwa jambo ambalo limezua utata kwa baadhi ya wachambuzi wa soka nchini huku wakitaka kamati hiyo kueleza ni kigezo gani kinetumika katika kuchagua mchezaji Bora.

Advertisements