Advertisements

Mama wa msanii Nandy ametoa neno lake kuhusu ndoa ya Billnass pamoja na mwananye Nandy, ameeleza kuwa kwa sasa wawili hao bado ni watafutaji hivyo wanapaswa kutulia kwanza mpaka wafikie malengo yao ndipo waingie katika ndoa.

Akizungumza kupitia EATV na EA Digital Radio amefunguka na kusema kuwa wakiingia kwenye ndoa kuna watoto na kuanzisha familia, hivyo itawarudisha nyuma kibiashara.

“Bado wote ni watafutaji, wasogee kwanza kutimiza malengo kisha waingie kwenye ndoa ipo tofauti siyo kama unafanya vitu vyako mwenyewe wako pamoja na wanashirikiana kwa vitu vingi hivyo wakae pamoja na wajipange ukiingia kwenye ndoa kuna kupata watoto na kuanzisha familia hivyo itawarudisha nyuma kibiashara” amesema Mama Nandy

Nandy akizindua Nandy Bridal
Advertisements

Aidha Mama Nandy amesema kuwa anajua walifanyiana suprise ya kuveshana pete lakini wao kama wazazi hawaitambui na lazima itarudiwa na kama wakitaka kufunga ndoa lazima michakato mingine ifuate kama kawaida.

Ikumbukwe hivi karibuni tu Nandy alifanya uzinduzi wa kampuni yake mpya ya Nandy Bridal >>>> Nandy azindua kampuni yake mpya ‘Nandy Bridal’ (+Video)

Advertisements

Unaweza kujiunga nasi kwa kusubscribe hapa chini
You can join us by subscribing here