Advertisements

Baada ya Harmonize kutangaza uzinduzi wa tamasha la Harmo Night Carnival ambalo litafanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Mkurugenzi wa kituo cha EFM na TVE Majizo amesema kuwa hajawahi kuona Carnival ikifanyika hapa nchini na hivyo atamsaidia Harmonize kwa kuongeza vifaa.

Mbali na Majizo B Dozen naye ameibuka na kumpongeza Harmonize huku akisema kuwa yeye ni mzoefu wa matamasha na shows nyingi sana lakini kwa alichokiandaa Harmonize ni kitu kikubwa sana hivyo anatamani siku ifike.