Luc EymaelMICHEZO

TFF yatoa adhabu kali kwa aliyekuwa kocha wa Yanga

Advertisements

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Nchini TFF imetoa adhabu kali kwa aliyekuwa kocha Mkuu klabu ya Yanga Africans, Luc Eymael baada ya kukutwa na makosa ya uchochezi na ubaguzi.

Kamati hiyo imeamua kumfungia kocha huyo kwa muda wa miaka miwili na kumtoza faini ya jumla ya Tsh Milioni 8 kutokana na makosa hayo.

Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF Alex Mashumbuzi amesema kuwa wameridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi ya kocha huyo na ataanza kutumikia adhabu hiyo hivi leo.

Advertisements

Aidha Mjumbe Mashumbuzi amesema kuwa Kocha Luc Eymael ambaye kwa sasa tayari ameshafukuzwa kazi na klabu aliyokuwa akiifundisha, ana haki ya kukata rufaa katika ngazi za juu za TFF (Kamati ya Rufaa TFF) endapo hatoridhishwa na adhabu iliyotolewa.

Ikumbukwe kuwa tuhuma zinazomkabili Eymael ziliibuka baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara uliopigwa na Yanga dhidi ya Lipuli ambapo Yanga iliibuka mshindi wa goli 1 dhidi ya Lipuli 0, Mechi iliyochezwa uwanja wa Samora Mkoani Iringa.

  Categories: MICHEZO

  Tagged as:

  Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google photo

  You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  Connecting to %s

  This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.