HABARI

Rais wa Ufilipino asisitiza kuosha barakoa kwa petroli

Advertisements

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejelea matamashi yake na kusema kuwa hatanii- “Kile nilichosema ni cha kweli ikiwa pombe haipatikani, hasa kwa maskini nenda tu kituo cha petroli na utumie petroli kuua vijidudu.”

Rais Duterte alisema maneno hayo mapema wiki iliyopita lakini maafisa wake walijitokeza na kumrekebisha kwa kusema kuwa alikuwa anatania na kueleza kuwa barakoa ziizotengenezwa kwa kitambaa zioshwe kama kawaida na zile zingine zitumike mara moja na kutupwa.

Lakini siku ya ijumaa Rais huyo alisisitiza matamshia yake na kuongeza “kile nilichosema ni ukweli nendeni kwenye vituo vya petroli”

Advertisements

“Wakosoaji wanasema Duterte ana kichaa, ni mpumbavuikiwa mimi ni mpumbavu wewe unastahili kuwa rais sio mimi”

Kile nilichosema ni cha kweli ikiwa pombe haipatikani hasa kwa maskini, nenda tu kwenye kituo cha petroli na uitumie petroli kuua vijidudu.”

“sio utani sio mzaha wewe jitahidi kuwa na mawazo kama yangu” Alimalizia rais Dutrte.

KIPI ALIKISEMA WIKI ILIYOPITA?

Bwana Duterte alisema kwamba wale ambao hawana vifaa vya kusafiishiabarakoa zao wanaweza kutumia petroli kuoshea barakoa zao.

Advertisements

“Mwisho wa siku tundika barakoa yako na unyunyize dawa ya kuzuia na kuua bakteria ya Lysol kama una uwezo (Lysol ni moja kati ya dawa maarufu ya kuulia bakteria nchini humo).

Baada ya matamshi hayo Msemaji wa serikali bwana Harry Roque alijitokeza mara moja na kumrekebisha “Siwezi kuaminin kwamba baada ya miaka minne ya urais bado hujui- ni utani tu kwanini tutumie petroli kuosha kitu?” amesema Bwana Roque kwa mujibu wa mtando wa Rappier

Categories: HABARI

Tagged as: , ,

1 reply »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.