HABARI

Makonda aaga rasmi ‘Ningekuwa jeshini ninazo medali za kivita’

Advertisements

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amekabidhi ofisi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa sasa Aboubakar Kunenge, kwa kushukuru kuwa mwendo ameumaliza kikamilifu na salama.

Aidha Makonda amesema kuwa hashtushwi na maneno ya watu yanayoendelea kumuandama kwani anatambua kuwa wanaofanya vizuri siku zote ndio husakamwa kwa maneno.

YOU MAY LIKE

Masaa 36 ya mfungwa namba 8612- Doug Korpi

Mwezi Agosti mwaka 1971, Profesa na mtafiti wa masuala ya Kisaikolojia Phillip Zimbardo akishirikiana na Ofisi za Navy za USA aliandika Tangazo ambalo lilibandikwa kwenye kila kona ya mji wa Calfornia. Tangazo […]

Advertisements

Makonda ameitoa kauli hiyo leo Agosti 3 katika makabidhiano ya ofisi hiyo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa watu wasihangaike kuwa yeye ataishi wapi bali waumie siku wakisikia amemuacha Yesu.

“Mwendo nimeumaliza, imani na kiapo changu cha utumishi nimekamilisha kikamilifu sasa, wana Dar es salaam mniruhusu nikapumzike kwa amani na kumlea vizuri Mkewangu kipenzi Maria na mtoto wangu Keagan” amesema Makonda

“Ningekuwa ni Jeshini ninazo medali za kivita ni askari mmoja aliyepo back bencher mwenye uwezo mkubwa wa kupigana vita vyovyote, mkinihitaji katika mapambano ya kumlinda Rais Magufuli hata kama ni saa 9 usiku nitanyanyuka” ameongeza Makonda.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.