MICHEZO

Papy Tshishimbi kuondoka Yanga

Advertisements

Papy Tshishimbi nahodha wa klabu ya Yanga amesema kuwa endapo klabu hiyo haitampatia mkataba mwingine yupo tayari kuondoka na kurejea nyumbani.

Kizungumkuti kuhusiana na mkataba wake kimezidi kushika kasi kwani mpaka sasa mkataba wake umebakiza siku 10 tu kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrik alisema mkataba wake utaishia Agosti 12.

“wao wanaweza kuachana na Papy leo sawa, naweza kupata timu nyingine ndani ya Tanzania ama nikakosa timu hakuna tatizo, kwani nyumbani nimeua? hapana nitarejea nyumbani. Amesema Tshishimbi.

Advertisements

Aidha Katibu alisema kuwa amempa mkataba Tshishimbi na kumtaka asaini ndani ya siku 14 na akishindwa kusaini dili hilo basi aondoke.

“Nimesikia yote ambayo Katibu amesema hakuna mtu ambaye anaweza kufanya masuala ya mkataba na akapeleka kwa vyombo vya habari kwamba Papy amepewa siku 14 asaini mkataba kwa kuwa wao wameongea sawa ninakubali lakini kwanini hawakuongea na Papy? Alimalizia

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na Tshishimbi ili wakifika kwenye makubaliano aongeze mkataba.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.