Advertisements

Msanii wa muziki wa bongo fleva Rich Mavoko ametangaza ujio wake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Rich amekuwa kimya kwa takriban miezi kumi baada ya kuachia kwa mara ya mwisho nyimbo yake ya Babilon, Ukimya aliokuwa nao Rich Mavoko unatafsiriwa kama maandalizi ya EP hiyo ambayo inaelezwa kuwa itakuja kufanya vema sokoni na mabadiliko makubwa sana hasa kwenye muziki wake Mavoko.

Akiandika kupitia ukurasa wake wa instagram Rich ameandika kuwa “nimewakumbuka watu wangu”

Advertisements

EP hiyo inatarajiwa kuachiwa tarehe 07 mwezi Agosti, 2020 katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es salaam.