Ilipoishia…

Sikuamini nilichokiona mumewangu yupo na bestman wake wakishiriki tendo, sikuamini macho yangu kibaya zaidi niliona mumewangu ndiye aliyekuwa kama mwanamke katika mchezo ule nilidondoka chini nguvu ziliniishia...

Sasa endelea..

Nilikaa kimya kwa zaidi ya dakika 15 bila ya kujitanmbua, nilijihisi mfu kwa muda mfupi, mapig ya moyo wangu nilihisi yamesimama kabisa, sikuamini kama nimeolewa na shoga, ndipo hapo nikaanza kutambua kwanini mume wangu hawezi kufanya vizuri akiwa namimi kitandani.

Nilibaki pale chini nikijililia peke yangu kwa kile nilichokuwa nimekiona, sikutaka kuamini kabisa kuwa mume wangu ni shoga na anashiriki mahusiano na mwanaume mwenzake daah iliniumiza mno.

Ghalfa nilisikia gari likiwashwa, niliinuka haraka na kujificha mahali pengine ili nisije kuonekana, nikamuona bestman pamoja na mumewangu wangu wakiingia kwenye gari na kuondoka, nilitoka nilipokuwa n imejificha na kurudi ndani, nikaingia moja kwa moja chumbani na kulazimisha usingizi, akili yangu haikuwa sawa kabisa.

Nilianza kuhisi mikono ikinipapasa nilipokuwa usingizini, nikashtuka na kukuta Jason yupo juu yangu akiwa anaupapasa mwili wangu,nilimuangalia Jason huku machozi yakinitoka nilishindwa kumtazama kabisaa niliogopa na kumuona mkatili huku nikijiuliza kwanini amenioa, amenioa ili nije niteseke au, niliumia mno.

Advertisements

Jason alishangaa kuniona natokwa na machozi bila sababu aliponiuilza nilimjibu tu kuwa kichwa kinauma, alipouliza na hali ya mama yangu nilimwambia kuwa mama yu salama, Jason alitoka nje na kumpigia simu daktari aje kunifanyia matibabu, ila hata alipofika na kunipima siuonekana na ugonjwa wowote.

Hali ya upweke majonzi na kilio iliendelea kwa takribani wiki mbili tayari mwili wangu ulianza kudhoofu kutokana na hali hiyo Jason alipata wasiwasi sana kwani hakuna ugonjwa ambao nilikuwa naumwa, bali jambo nililokuwa nimelishuhudia kwa mume wangu ndilo lilikuwa ugonjwa tosha.

Siku moja baada ya kuona hali ile imenizidia na ingeweza kupoteza uhai wangu kwa masihara niliamua kumpigia simu daktari ambaye ni rafiki yangu pia nikamuomba kukutana naye mahali kisha nimueleze matatizo yangu.

Nilikutana nae kama tulivyopanga, nikamuomba kuwa nitakayomueleza pale yawe siri yangu mimi na yeye tu “Camilla mimi ni daktari nina siri nyingi sana… kazi yangu ni kutunza siri za wagonjwa wangu pia”. Daktari alienileza.

Nikaanza kumsimulia tangu mwanzo mpaka mwisho kuhusu mahusiano yangu na Jason, nilimueleza zaidi jinsi nilivyompenda mumewangu hata kama yuko hivyo nisingependa kumuacha aendelee kuharibika zaidi.

Dokta alinipa pole, kisha akaanza kunipa ushauri na jinsi ya kufuata alinipa faraja kuwa mumewangu anaweza kurudi katika hali yake ya kawaida kwani kama anaweza kufanya tendo kwa mara moja basi atakuwa hajaharibiwa kabisa.

Alichonishauri ni kwenda kuongea nae na kumepeleka hospitali kwake ili akapatiwe matibabu, nilimshukuru daktari kwa ushauri wake pamoja na matumaini aliyonipatia. Niliwaza ni njia gani ningeweza kumweleza mume wangu hata anuielewe.

Basi nilimuaga dokta na kuondoka nikapitia dukani kisha nikanunua suti nzuri sana kwani tayari nilishajua mume wangu anapenda suti nikaitia kwenye mfuko kisha nikapitia bar kupata kinywani ili kuweka akili yangu sawa na kutoa aibu, nikapata kinywaji kikali sana huku kikidhamiria kwenda kumweleza mumewangu kila kitu.

Nilipiga pombe mpaka nilipoona sasa niko fit kwenda kumweleza bila aibu wala uoga wowote, nilienda mpaka nyumbani nikamkuta mume wangu sebuleni akiwa ananisubiri.

Nikamchukua na kumpeleka chumbani, nikiwa sina aibu wala uoga juu yake moyoni mwangu nilijisemea liwalo na liwe leo nitammwambia akiniacha basi na iwe tu.

“mke wangu imekuwaje leo umekuywa pombe…” Jason aliniuliza

“Usijali utajua tu kwanini nimekunywa… “ Nilimjibu Jason

“Jason nisikilize kwa makini…  nitakayokuambia hapa si kwamba nakusingizia au eti ni kwasababu ya pombe nitakuambia ukweli kwasababu naumia kila siku ila usiponielewa nitaondoka kwani nimechoka kuvumilia….” Nilisema nikiwa na jazba huku machozi yameshaanza kunitoka

Advertisements

Nilianza kumwambia jinsi nilivyokuwa nikiwahisi yeye na rafaiki yake mpaka siku niliyowakuta, bila uoga nilimapasukuia Jason matendo yake yote nikaueleza kuwa ndio maana hawei kunipa tendo la ndoa kama inavyotakiwa, ndio maana anakosa nguvu za kuniridhisha mimi.

Nilimweleza mambo yote bla uoga kabisa niliamini pombe na ushauri wa daktari umenisaidia sana, mwishowe nilimueleza kama angependa kurudi katika hali yake ya zamani aniambie ili nimsaidie na kama hataki aniache mimi niende zangu kwani siwezi kuvumilia mateso yale.

Nilimuona Jason akitokwa na machozi tayari nikatambua kuwa nimemuweza kusema ukweli na umemuingia kwelikweli, aliinuka na kupiga magoti mbele yangu kwa mara nyingine na kuniomba msamaha kwa haya yote yaliyotokea pia aliniomba msamaha na kunileza kuwa yupo tayari kuacha mambo haya na amekuwa akitamani siku nyingi sana kuacha lakini hakuwa na msaada wowote ule.

Nilifuarhi kusikia vile hapo nnilitambua kuwa endapo ningefanya uamuzi wa kumuacha mume wangu basi ningekuwa nimepoteza na sio mke bora, nilimwambia kuwa alichokifanya ni kosa lenye adhabu kubwa mbele za Mungu hivyo anatakiwa kumuomba msamaha Mungu pia, nilimueleza kuwa kesho tungeenda hospitali ili akapate msaada wa kitabibu.

Usiku ule Jason alikubali kunieleza kila kitu alinambia kuwa alianza mchezo huo akiwa masomoni huko ulaya mpaka tabia hiyo ikakomaa, alianiambia kuwa hata nusu ya mali zake zote alizipata kwa njia hiyo.

Siku ule nyumba yetu ilijawa na majonzi tupu Jason alinileza kila kitu alianielewa kwa kila jambo nililomuambia, moyoni mwangu nilimshukuru sana daktari yule ambaye alinishauri kufanya hivo na sio kumuacha kwa siri mume wangu.

Asubuhi ilipofika nilimpeleka Jason kwa daktari ambaye ni rafiki yangu, sasa hapo pombe tayari ilishaisha kichwani mwangu aibu na uoga vilikuwa vimeanza kutawala akili yangu, nilifika hospitali na kumpigia simu rafiki yangu, naye alitulekeza kuwa tuende ofisini kwake, ambako ndiko matibabu yangefanyikia. Tuliiingia mimi na mume wangu, baada ya kusalimiana daktari aliniomba kusubiri nje ili aongee na mumewangu kiume zaidi nami siku mbishi nilitoka nje na kusubiri.

Nilikaa kama nusu saa hivi mume wangu alipatiwa matibabu, baada ya muda daktari aliniomba kuingia ndani, kwa ajili ya maelezo alitupatia maelezo ya vyakula ambavyo nilitakiwa kumpikia mumewangu pamoja na mazoezi aliyotakiwa kufanya, aliniambia pia tusikutano kwenye tendo kwa muda wa miezi miwli mpaka pale dawa alizompatia zitakapokwisha na kurudi hospitalini kwa uchunguzi zaidi.

Baada ya kutoka hospitali mume wangu aliniomba kwenda kwa mchungaji ili akafanyiwe maombi, nilifurahi sana kwani sikuamini kuwa angeweza kuniambia jambo lile hata kama tulikuwa tumelipanga, basi bila kuchelewa niliendesha gari mpaka kanisani, na huko tulimkuta baba mchungaji.

Mume wangu alimuomba kuongea naye kwa muda, hakuwa na aibu hata kidogo alimweleza kila kitu pamoja na nia yake ya kuomba msamaha mbele za Mungu, Baba mchungaji alinipa hongera kwa juhudi nilizozifanya kumuombea mume wangu na baba mchungaji alisisitiza kujitenga mbali na marafiki zake wote ambao walikuwa na tabia hiyo.

Tulifanya maombi kwa ajili ya kuomba msamaha mbele za Mungu kwa hali hile ambayo mumewangu alikuwa nayo, baada ya hapo tulirudi nyumbani.

Tukiwa njiani mume wangu aliniambia kuwa tayari ameshamuleza rafiki yake kuwa ule mchezo hauhitaji tena. Nilifurahia sana, zaidi aliniambia kuwa tutasafii na nichague nchi yoyote ile ya kwenda kwa ajili ya kukaa mbali na marafiki zake wote pamoja na kutumia dawa zake vizuri.

Advertisements

Muda wote alibaki akinishukuru kwa jinsi nilivyomkomboa kutoka katika dimbwi la uchafu hule, nilimwambia mumewangu kuwa natamani kwenda nae Dubai kwani nilikuwa nikisikia kuwa ndiye nchi yenye kila aina ye mahotel makubwa na mazuri sana.

Nilizani anatania lakini kumbe mume wangu alikuwa seriou kabisa, siku moja alirudi akiwa na tiketi mbili a ndege nlishangaa sana, niliinuka na kumkumbatia mume wangu nikamshukuru kwani nilijua fika itakuwa mara yangu ya kwanza kupanda ndege na kufika Dubai.

Siku ya safari ilipowadia sikuweza kulala kabisa nilibaki nikisubiri tu muda wa kupanda ndege ufike, mumewangu alibaki akicheka sana kwani yeye alikuwa tayari mzoefu kwani mara akadhaa alishapanda ndege.

Hatimaye ndoto yangu ikatimia kwa mara ya kwnza nikapanda ndege pembeni yangua akiwa mwanaume wa maisha yangu Jason, tulitua uwanja wa ndege wa Dubai International Airport

Tayari alishaweka mipango yote sawia ikiwemo hoteli tutakayofikia hivyo ilikuwa rahisi sana kwetu.

Maisha mapya katika nchi ya kiarabu watu wenye utamaduni tofauti na sisi niliyafurahia sana, nami sikusahau dhumuni la kuja kule nilihakikisha mumewangu anakula vizuri na anafanya mazoezi kama tulivyokuwa tumeambiwa na daktari, pamoja na kumeza dawa ambazo alipangiwa.

Daktari tuliendelea kufanya naye mazungumzo na alikuwa akitueleza kila tulichokuwa tunatakiwa kufuata kwa njia ya simu.

Baada ya miezi miwili tulirejea Tanzania kwa muda ili kuja kufanya check up, Daktari alituambia kwa mume wangu anaendelea vizuri na tayari ameshapona, alituapatia vidonge ambavyo alitakiwa kumeza kwa ajili ya kuwa salama kabisa.

Tuliamua kurudi tena Dubai kwa ajili ya kuendelea na maisha yetu huko, tayari nilishaanza kuona matunda ya ndoa yangu, baada ya miezi mitatu kupita mume wangu alianza kuwa na hisia nami, uwezo wake kitandani ukaogezeka maradufu, moyo wangu ulifarijika sana nikahisi kuifuarahia ndoa yangu tena.

Baada ya kukaa muda mrefu tuliamua kurudi tena nyumbani Tanzania ili kuendelea na maisha wakati huo tayari nilikuwa na ujauzito wa Jason jambo ambalo lilikuwa faraja na kiunganisho kikubwa cha ndoa YETU.

Advertisements

FUNZO

  • Ndoa ni safari ndefu yenye mambo mengi sana, unapoona mwenzio yupo katika tatizo kubwa ni vyema kumsaidia au kujaribu kutoa msaada na sio kuadhimia kumuacha kwa siri tu.

  • Si vyema kuingia kwenye ndoa ikiwa bado mmepitia kipindi kifupi sana cha uchumba wengi wanalia na ndoa zao kwani hawakujuana vizuri katika uchumba wao

  • Miasha ndani ya ndoa ni siri ya wanandoa hivyo ni vyema kushauriana kabla ya kuyatoa nje kwa walimwengu

  • Msamaha ni moja kati ya nguzo muhimu sana katika ndoa #tusameheane na kuanza upya