ANGALIZO Majina yote yaliyotumika katika chombezi hii ni majina ya kufikirika tu, hayajalenga kumtaja mtu yeyote.

Ilipoishia…

“Jason pls kwanini lakini unanifanyia hivi… aaah… why Jason!!” Nilimuuliza Jason huku machozi yakinitoka

“Camilla nakuomba unipe nafasi nibadili maisha yako, ebu angalia jinsi itakavyopendeza ukiwa mama nami nikawa baba ebu angalia mawanda ya mapenzi yatakavyokuwa hayana kikomo tafadhali nipe nafasi Camilla….”

Advertisements

Sasa endelea….

Nilibaki nimejiinamia chini sina la kufanya msururu wa maswali yasiyo na majibu yalijaa akilini mwangu, nilibaki kama askari anayetaharuki akiwa vitani asijue la kufanya!!… Ni kweli Jason ni mwanaume mzuri na shupavu kwa mali na akili, anacho kila kitu ambacho msichana yeyote aliye timamu asingeliweza kumkataa.

Niliinua uso wangu na kuutazama uso wake ambao sasa ulishaanza kuonyesha hali ya huruma, nilipiga moyo konde nikajisemea moyoni hii ni hali ambayo kila mwanaume huonesha hapo tayari nilishakumbuka yaliyonikuta huko mwanzoni.

“Jason nimekuelewa ombi lako… ila nahitaji muda kuwaza kwa kina..” Nilimwambia

“Camilla haijalishi muda gani unahitaji… sitochoka kuwa mvumilivu kukamilisha ndoto zangu kwangu”

“Nitakusubiri tu Camilla mpaka utakapokuwa tayari..” Jason aliniambia huku akitia huruma sana.

Tayari nilishaona tuwi la nazi limeingia nzi niliinuka na kumnyanyua Jason mahali alipokuwa amepiga magoti kisha nikamuomba arudi kuketi kwenye sofa, hapohapo bila kuchelewa nikaanza visingizio vya kutaka kuaga niondoke nyumbani.

Akili yangu ilikuwa haijatulia kabisa, niliamua kumuaga Jason nirudi nyumbani hakuwa na budi kwani tayari huzuni na machozi vilishatawala ukumbini pale hivyo ilimbidi tu aniruhusu, alinipeleka mpaka kwenye gari tukaingia kisha tukaanza safari ya kunirudisha nyumbani.

Njia nzima kimya kilitawala Jason alijaribu kuniongelesha mara chache lakini bado akili yangu haikuwa pale kabisaa…

Alinipeleka mpaka nyumbani, kabla sijashuka ndani ya gari Jason alitoa kibunda cha fedha na kunikabidhi kisha akaniambia “hizi zitakusaidia siku mbili tatu..”.

Nilizipokea shapuu kwani ni muda mrefu sana tangu nishike pesa nyingi kiasi kile.. nilimuangalia Jason bado nilishindwa kuelewa nia yake hasa kwangu ni ipi, ni mapenzi tu ama kuna kingine..?.

Niliachana na Jason mahali pale nikaingia chumbani kwangu na kujilaza kitandani moja kwa moja kisha usingizi ukanichukua.

Siku iliyofuata kama ilivyokuwa kawaida yangu asubuhi na mapema niliamka, ili kujiandaa na kazi zangu tayari pesa ambayo nilipatiwa na Jason nilishaiingiza kwenye biashara yangu ya kuuza mihogo, ilikuwa pesa nyingi hivyo sikuona sababu ya kuitumia vibaya.

Advertisements

Asubuhi na mapema Jason tayari alishanitumia meseji kama ilivyokuwa kawaida yake, safari hii alikuwa akiulizia jibu lake, bado niliendelea kumzungusha tu ili nitambue kama kweli ananipenda au basi alitaka kunichezea tu.

Nilifika kazini kwangu, kwa kuchelewa siku ile hivyo nilikuta baadhi ya wateja wangu wameshapata kifungua kinywa mahali pengine, wahenga husema siku njema huonekana asubuhi, biashara yangu haikuwa nzuri sana kwa siku ile. Nilivumilia huku nikijipa imani kuwa ipo siku namimi nitafanikiwa zaidi ya pale nilipo.

Iilpofika jioni nilianza safari kurudi nyumbani kwa ajili ya kuendelea na mambo mengine, niliposhika simu yangu ya mkononi nilikuta missed calls nyingi sana za Jason pamoja na marafiki zangu wengine, sikuwa na la kujibu nilihisi ningekuwa nimemuudhi sana kwa kushindwa kupokea simu yake.

Nilipofika nyumbani nilikaribishwa na ujumbe kutoka kwa mama mwenye nyumba

“Mwanangu kuna rafiki yako alikuja hapa…” Mama aliniambia

“MMH… Yupi huyo mama mbona unanitisha…!!” Nilimjibu mama mwenye nyumba kwa mshangao

“MMH!! hakujitambulisha kwa jina ila ameacha mzigo ngoja nikupatie…” Mama aliniambia

Aliingia ndani na kutoka akiwa ameshika mifuko miwili, nilipoiangalia nilijua ni mifuko ya supermarket kabisaaa, alinikabidhi na kuniambia amesema ukiipata umjulishe..!!

Niliingia ndani bila hata kupumzika nikaanza kuifugua ile mifuko, kwa mshangao nilianza kukutana na karatasi lililopambwa nilipolifungua nikatambua kuwa ni Jason baada ya kuona jina lake pamoja na ujumbe ulisomeka “NAKUPENDA CAMILLA”.

Ndani ya mifuko mingine nilikuta nguo nzuri sana nilizijaribu zilikuwa zimenikaa vema hata nikajiuliza mmh Jason anaijuaje size ya nguo ninazovaa.

Niliamua kumpigia simu ili nimshukuru kwa zawadi alizonilietea,

“Hallo Jason… hali yako..? Niliuliza

Camilla subiri nikupigie mama…!!” Jason aliniambia

Alikata simu na kunipigia tena kisha tukaanza kuongea aliniambia jinsi alivyokuwa akinikipigia simu na sikupokea simu zake, nilimuomba msamaha kwa halililotokea naye akanielewa nilimshukuu kwa zawadi alizoniletea nilitaka kujua kwa jinsi gana huwa anaweza kunipa nguo ambazo huo zinanikaa vizuri kabisa, akaniambia kuwa alishawahi kuwa dizaina wa nguo za wadada nilicheka tu.

Usiku ule nilitamani kumjibu kuwa nampenda pia, ila nilisitisha zoezi hilo niliona kama atanihisi mtu rahisi sana kumwambia kwa njia ya simu, hivyo bado niliendelea kusubiri tu mpka pale muda utakapofika.

Hali ile iliendelea mpaka wiki nzima ikaisha Jason hakukata tamaa kuimba nakupenda mbele yangu, kila aliniona alizidi kunieleza tu jinsi alivyokuwa akinipenda.

Siku moja niliamua kumsuprise Jason, niliamua kwenda mpaka nyumbani kwake baada ya kutoka kazini kwangu, nilifika kwake nikagonga geti mlinzi alikuja kunifungulia alishangaa sana kuniona  peke yangu.

Advertisements

Alinikaribisha ndani haikuwa shida kwani tayari alikuwa ameshanifahamu, nilipita moja kwa moja mpaka sebuleni kisha nikajikaribisha mwenyewe

Alipofika mfanyakazi nilimuomba aniitie boss wake ambaye ndiye Jason, haukupita muda mrefu Jason alifika mahali pale naye alishangazwa sana kuniona nyumbani kwake bila ya kutegemea.

Kabla ya kumjibu neno lolote niliinuka na kwenda kumbusu Jason nikimaanisha kuwa ombi lake tayari nimeshalikubali alifurahi sana muda kidogo nilimuona mwanaume mwingine akitoka chumbani mwa Jason akiwa kifua wazi, nilishangazwa kwani hata Jason naye alitoka akiwa kifua wazi hivyohivyo, alifika na kunisalimu kwa bashasha.

Niliitikia salamu yake pia, nilimuona akivaa shati lake kisha akaaga na kumwambia Jason “ngoja nikuache basi na shemeji kazi yetu tutamalizia badae” naye akaondoka, nilimsogelea zaidi Jason na kumuuliza ni nani yule anatoka chumbani kwake akiwa vile, naye akanijibu kuwa ni rafiki yake kipenzi wa muda mrefu sana na wamekuwa wkishirikiana katika mambo mengi hasa ya kiofisi.

Nilimuelewa Jason sikutaka kung’ang’ania sana kwani sikuwa nimeliendea hilo kwa siku ile, kwa mara ya kwanza nilikaa nyumbani kwa Jason mpaka usiku ulipofika ndipo akanirudisha nyumbani.

Mapenzi yetu yalizidi kukua kwa kasi sana sehemu yangu ya kazi ghafla ilibadilshwa na Jason ikafanywa kuwa yenye hadhi ya juu zaidi, ukawa mgahawa mzuri na maarufu sana miezi miwili tayari ilishapita tayari tukwa ndani ya mapenzi yetu.

Kila kitu kilionekana shwari kabisa, Jason aliyabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana alinifanya kuwa malkia wa moyo wake kiasi ambacho sikutegemea, nami nikawa mmoja kati ya wanawake wenye hadhi ya juu, kila nilichohitaji nilipata toka kwa Jason tena kila kitu nilipata kwa zaidi ya nilivyoomba.

BAADA YA MIEZI SITA

Siku moja niitamani sana kukutana na mpenzi wangu Jason hivyo niliwahi chumbani kwake kabla ya yeye kurejea kutoka kazini, nilikuwa nimebeba maua ya kila rangi nzuri yenye kuvutia, pamoja na mishumaa yenye rangi tofauti tofauti.

Nilikipamba chumba vizuri sana tayari kwa ajili ya usiku mrefu pamoja naye, nilipomaliza shughuli hiyo niliingia jikoni mwenye na kumuandalia chakula kizuri sana ambacho nilijua wazi kuwa kingemuongezea nguvu za kutosha nilitamani sana kuwa pamoja naye usiku ule.

Advertisements

Nilipomaliza nilikaa na kumsubiri Jason arudi kutoka kazini, nilisubiri sana mpaka saa tatu usiku ndipo akarudi, sikujali kuchelewa kwake nilienda na kumkumbatia mpenzi wangu kisha nikamkaribisha, nilimuandalia maji ya kuoga kabla hajaingia chumbani ili asije akaona jinsinilivykipamba chumba.

Baada ya kuoga alikuja mezani nikaweza kushiriki naye chakula cha usiku. Tuliongea mengi kuhusu kazi zake, nilipa pole pia kwani ndiyo kutafuta huko.

Baada ya muda mchache tulimaliza kula chakula hatimaye sasa dhumuni langu usikuule lilikaribia kutimia kwani Jason alinibeba mikononi mwake na kunipeleka chumbani.

Tulipofika chumbani alishangazwa sana na jinsi kulivyobadilika maua mekundu kwa meupe pee, harufu nzuri na mishumaa tupu wala hamna taa iliyowasha, nilimwambia kuwa mpenzi wangu naomba nilishiriki usiku wa kwanza nawewe siku ya leo natamani sana mpenzi wangu!!..

Tulipanda kitandani kwa ajili ya kuanza safari yetu, ghafla nilianza kumuona Jason akiwa amebadilika sura yake imeanza kuonesha huzuni, nilishindwa kuelewa kwanini nilipomuuliza aliniambia kuwa ni stori ndefu ila angeomba siku ile tusifanye chochote balia akuwa ameipanga kuniomba jambo fulani, moyo wangu uliniuma lakini sikuwa na budi nilimwambia kwa kuwa ni jambo la kuongea tu wacha nikisikilize tu, huku nikijiba imani kuwa tutaendelea baada ya maongezi hayo…

“Camilla naomba unielewe natamani… natamani sana nikuoe hata leo hii nipo tayari”

“Jason najua unatamani kueleza upendo wako kwangu kwa vitendo, lakini angalia ni miezi sita tu tangu nikujue….” Camilla alijibu.

“Camilla miezi sita!! miezi sita ni mingi kumtambua mtu na tabia zake isitoshe mimi nimekufahamu wewe muda mrefu mno kabla hata hujanijua…tafadhali nakupenda Camilla” Jason alizidi kuchimbia msimamo wake.

Advertisements

“Jason kwanini unatamani kunioa mapema hivi?” Camilla aliuliza

“Camilla mpenzi wangu… maisha ni mafupi mno natamani nikae nawe angalia tayari nina nyumba nzuri nina magari lakini sina mke,..!! halafu pia nikikuoa nitakujengea heshima mpenzi wangu wewe hulioni hilo? Jason alieleza.

“Jason sawa nimekuelewa lakini.. laklni naomba basi muda kidogo nifikiri juu ya hili tafadhali mpenzi wangu..”

“Camilla nilijifunga nisifanye chochote na wewe mpaka nitakapokuoa… ili nikujengee heshima kwako mpenzi wangu”

Jason aliongea huku akiwa na kigugumizi nilianza kuhisi kuna shia juu yake lakini sikutaka kuliongea hilo kwake nilinyamaza kimya nililala huku machozi yakinitoka naye akinibembeleza tu.

Ilipofika asubuhi kabla hajaenda kazini nilimjibu kuwa nimemkubalia omi lake ila taratibi zinabidi zifuatwe kama inavyoakiwa.

Palepale Jason alifurahi na akaghairi kwenda kazini kisa akaniambia kuwa yupo tayari kufuata taratibu zote zinzotakiwa kufuatwa hivyo nimpe maelekezo tu ya kipi cha kufanya, niliona fuaraha ambayo sikuwahi kuona usoni pake nilifurahi kumuona hivyo nilijuwa kuwa suala la ndoa alikuwa akilisubiri kwa muda mrefu sana.

Aliniomba kuarika marafiki zangu kwa idadi yoyote nitakayopenda, huku naye akikaribisha marafiki zake ambapo rafiki yake ambaye huwa namuona mara nyingi ndiye aliyemfanya kuwa bestman wake.

NDOA

Mbele ya kanisa pamoja na wazazi wetu tuliweka kiapo, kuwa mimi na Jason tutakuwa mke na mume kwenye shida na raha, mchungaji alitufungisha ndoa hatimaye ndoto yangu ya kuolewa na kuishi na mume wangu ikatimia kama ilivyokuwa Jason alivyotamani kunioa mimi ilitimia.

Sherehe ilifana sana kama ambavyo tulikuwa tumeipanga ilienda hivyo hivyo.

Usiku wa kwanza wa ndoa yetu, niliona kabisa kama nazaliwa upya kukutana na mume wangu, kama kawaida yangu nilipamba chumba chetu vizuri sana, safari hii niliongeza vitambaa na ujuzi zaidi hakika nilitamani Jason afurahie usiku huu.

Safari hii ilikuwa kama nilivyotegemea Jason alinipa kile kitu moyo wangu ulikuwa unahitaji japo ilikuwa ni mara moja tu, na hakuweza kurudia tena tendo, nilishanga na kujiuliza mwenyewe ni kwanini imekuwa hivi wakati siku nyingi sana hatuajakutana, nilianza kuhisi labda ana mwanamke mwingine lakini nikajisemea hapana kwani nimekuwa naye siku nzima.

Advertisements

Nilijiapiza kutafuta sababu ya hili kwani hata nilipomuuliza hakutaka kunipa jibu lolote, alibaki kusema tu hata naye hajui kwnini imekuwa hivyo, aliniomba msamaha sana kwa kuwa nilimpenda sana mumewangu sikuwa na budi kumsamehe tu.

Asubuhi na mapema niliamka na kwenda kumuaga mumewangu wangu kuwa naenda hospitali aliniomba anisindikize kwani bado tupo ndani ya siku saba za fungate, nilimstopisha na nikamuomba niende mwenyewe tu haikuwa rahisi lakini mwishowe alikubali, nikamuaga kuwa ningechukua muda kidogo.

Nilifika kwa daktari ambaye alikuwa rafiki yangu tangu tukiwa tunasoma ili kumueleza tatizo la mumewangu na nione msaada wake kitaalamu, alinieleza mambo mengi sana akaniambia huenda ni hofu tu ndo imemfanya mumewangu apoteze hamu ya tendo la ndoa hivyo nimsubirie kwa muda mpaka anizoee huenda hali ikabadilika, pia alinishauri kushiriki naye tendo mara kwa mara ili kumuondoea hofu hiyo.

Nilimshukuru kwa msaada wake namimi nikarudi nyumbani,nilifika nyumbani na kuingia ndani sebuleni moja kwa moja, nikawakuta mumewangu pamoja na rafiki yake ambaye ndiye alikuwa bestman wake waliponiona walishtuka sana nami nilishangaa kuwaona wameshtuka sana..

“mkee–ee-wangu si ulisema uta-e-chelewa ku–r-udi nyumbani…!!” Jason aliuliza kwa mshangao.

“ndio lakini daktari sikumkuta ndo mana nimewahi kurudi mumewangu…!!” Nilimjibu huku nikiwa na wasiwasi kidogo.

“ooh– oh s–sawa hamna shida mpenzi karibu–..” Jason alinikaribisha huku akionekana mtu mwenye  hofu kidogo…

“Karibu shemu ukae.. tulikuwa tukiongea masuala ya kazi na Bwana Jason hapa…. umetushtua kuingia ghafla.. haha haha..!! Bestman wake aliniambia

Nilicheka kidogo na kumwambia kuwa asijali wacha mimi nikaendelee na shughuli zangu za jikoni, japo niligundua kuwa kicheko kile ni cha kinafki bado nilibaki na dimbwi la mawao kwanini walishtuka pale..

Hali hii iliendelea mpaka mwezi ukapita nilijaribu kumpa mara nyingi mumewangu kama daktari alivyonishauri lakini bado hali ilionekana vilevile tu hamna chochote kilichobadilika, mbaya zaidi mumewangu alikuwa na rafiki yake mmoja tu ambaye niliweza kumtambua nilitamani kumfuata anisaidie lakini nayeye hakuwa ameoa hivyo niliona si vyema kumshirikisha masuala ya ndoa mtu ambaye hajaoa.

Siku moja niipanga kugundua kwanini kila nikitoka tu basi rafiki wa mumewangu huja nyumbani na kila nikirudi huwa wanakuwa kwenye hali ya wasiwasi sana hivyo nikaandaa mpango wangu mwenyewe.

Siku ya jumamosi asubuhi nikamuaga mumewangu kuwa mama nyumbani anaumwa hivyo naomba ruhusa nikamuone nitawahi kurudi kabla giza halijaingia.

Mume wangu alinikubalia bila pingamizi lolote nilitoka nyumbani na kwenda nyumba ya jirani kwa shoga yangu tofauti na nilivyoaga nilikaa kwa muda wa nusu saa huku macho yangu yote yakiwa nyumbani kwangu nione labda mumewangu atatoka nyumbani au kuna mwanamke ataingia nyumbani.

Baada ya muda mrefu wa kusubiri niliona gari aina ya Prado nyeusi ikiwa inaingia nyumbani kwetu, sikuweza kuona nani alikuwemo ndani ya gari ile, kwani ilikuwa tinted kabisa. Nilisubiri kama dakika ishirini hivi kisha nikajipanga kuwa nakwenda kumfumania huyo ambaye huwa anashare mume na mimi, roho yangu ikiwa imejaa jazba ya pambano kabisaa.

Nilitembea mpaka getini kisha nikaingia ndani na kuzunguka mpaka nyuma ya nyumba, nikaenda mpaka dirisha la chumbani kwetu, nilipochungulia sikuweza kuona mtu yeyote yule, kisha nikachungulia dirisha upande wa sebuleni sikuweza kuona mtu yeyote.

Nilibaki nikijiuliza huyo mtu ameingia wapi, nilisogea mbele mpaka chumba cha wageni kisha nikachungulia….

“looh Mungu wangu….!!!!.. siamini macho yangu…!!..”

Sikuamini nilichokiona mumewangu yupo na bestman wake wakishiriki tendo, sikuamini macho yangu kibaya zaidi niliona mumewangu ndiye aliyekuwa kama mwanamke katika mchezo ule nilidondoka chini nguvu ziliniishia…

Bofya hii link ili kuendelea>>> Chombezo: Mume wangu ni mume wa bestman wake! 3 (Mwisho)