Advertisements

Mtanzania Saniniu Kuryan Laizer ambaye hivi karibuni aliibuka kuwa bilionea baada ya kupata mawe ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 7.8 amegundua jiwe lingine tena lenye thamani ya mabilioni.

Baada ya kupimwa imejulikana kuwa jiwe hilo lina uzito wa kilo 6.33 na thamani yake inatarajiwa kutangazwa baada ya kuthaminishwa kwa jiwe hilo.

Madini ya Tanzanite
Advertisements

Jiwe la sasa hivi alilolipata Laizer linasemekana kuwa ni jiwe la pili kwa ukubwa kuwahi kupatikana katika machimbo hayo kaskazini mwa Mirelani.

Mwezi mmoja tu uliopita Laizer alipata madini kama hayo mawili ambapo moja lilikuwa na uzito wa kilo 9.2 na thamani ya shilingi bilioni 4.5 pia lingine likiwa na uzito wa kilo 5.8 ambayo thamani yake ni bilioni 3.3.

Serikali inatarajiwa kukabidhiwa jiwe hilo la Bwana Laizer ambapo pia atakabidhiwa fedha zake kutokana na thamani ya jiwe hilo.

Saniniu Laizer mwenye umri wa miaka 52, ni mume wa wanawake wanne na amejaliwa kupata watoto 30.

Bwana Saniniu Kuryan Laizer

Kupitia mtandao wa twitter Wizara ya madini ya Tanzania inamtambua Bwana Laizer kama bilionea pia kwa mujibu wa Wizara hiyo inaeleza kuwa madini yenye uzito wa namna hiyo hayakuwahi kupatikana katika machimbo ya Tanzanite ahapoo awali.

Madini aina ya Tanzanite huchimbwa nchini Tanzania pekee.