Advertisements

Rais wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo kufuatiwa na kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa.

Kupitia barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli ametangaza kuanzia Julai 24 kutakuwa na maombolezo ya siku saba na bendera itapeperushwa nusu mlingoti, pia amewasihi Watanzania kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.