Advertisements

Wanasayansi wanasema wamefanya uchunguzi kwa vinasaba sita vya popo duniani, na wamegundua kuwa maisha yao yanajumuisha kidokezo cha vinasaba vyao vinavyowafanya kuwa na kinga ya kipekee inayowalinda dhidi ya virusi vya corona.

Pia katika utafiti huo wanasayansi wana matumaini ya kufahamu jinsi popo wanavyoweza kubeba virusi vya corona na kuvisambaza bila wao wenyewe kupata maambukizi yatokanayo na virusi hivyo.

Bofya kusoma pia…

Advertisements

Wanasema kuwa huenda utafiti huo ukaweza kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa kutoa suluhu ya kudumu kusaidia afya ya mwanadamu.

Profesa Emma Teeling kutoka chuo kikuu cha Dublin amesema kuwa uchunguzi walioufanya katika chemebe za urithi umeweza kubaini kuwa popo wana mifumo maalum ya kinga mwilini mwao.

Aidha ameongeza kuwa endapo wataweza kuelewa jinsi popo wanavyoweza kubeba virusi vya corona bila kupata maambukizi inaweza kuwasaidia katika upatikanaji wa tiba mpya ya ugonjwa wa covid 19 kwa binadamu.

“Ikiwa tunaweza kuiga kinga ya popo dhidi ya virusi, unaweza kupata tiba. Tayari imeshabadilika na kukua kwahivyo sio kwamba uvumbuzi unaanza mwanzo, sasa tuna vifaa vya kutuwezesha kutambua hatua tunazohitajika kuchukua tunahitajika kuvumbua dawa ili kufanikiwa”

Profesa Emma Teeling ameiambia BBC
Advertisements

Profesa Teeling ni mwanzilishi wa mradi wa Bat1K Project ambao unalenga kuchunguza vinasaba vya popo 1,421 waliopo hai duniani.

Vinasaba hivyo ndivyo vinavyohitajika ili kuweza kubaini suluhu ya kijenetiki ambayo inaweza kuboreshwa zaidi na hatimaye kuwa kusaidia kukabiliana na magonjwa kwa binadamu.

Spishi sita zinazochunguzwa ni popo aina ya horseshoe kwa kingereza ni jamii ya Rhinolophus Ferrumiquinum, Egyptian fruit jamii ya Rousettus Aegyptiacus popo aina ya Spearnosed jamii ya Phyllostomus discolor, popo aina ya grater mouse eared jamii ya Myotis myotis, popo aina ya Kuhi’s Pipistrella jamii ya Pipistrella kuhii na popo velvety free tailed jamii ya Molossus molossus.

Wanaikolojia na wahifadhi wa Mazingira wameonya kwamba popo wasiuliwe. picha na BBC-Swahili
Advertisements

Ugonjwa wa covid 19 unasemekana kwamba chimbuko lake n popo ambapo ulisambaa kutoka kwao mpaka kwa binadamu pia magonjwa mengine kama vile SARS, Mers na Ebola yanasemekana kuwa yamesambaa kwa bindamu kupitia njia hiyohiyo.

MAMBO YAPI MENGINE UCHUNGUZI UMEBAINI?

Timu ya Kimataifa ya Utafiti kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya hali ya juu imeweza kubaini pia.

  • Kwa kulinganisha kundi hilo dhidi wanyama wengine wanaonyonyesha 42 waliweza kujua maisha ya popo.

  • Popo wanaonekana kuwa karibu na kundi la wanyama walao nyama (mbwa, paka nyangumi, kakakuona na wanyama wenye kwato.

Advertisements
  • Uchunguzi wa jenetiki zao pia ulibaini chembe ambzao huenda zinzchangia mwangwi wa sauti zao ambazo popo hutumia kuwinda na kutembea katika maeneo yenye giza totoro

  • Kukokotoa utofauti wa jinetiki kulibaini chembe za urithi ambazo zimekuwa na mabadiliko tofauti kwa popo jambo ambalo huenda linachangia uwezo wao wa kipekee