Advertisements

Mwanamuziki wa bongo fleva Nandy ambaye pia ni maarufu kama The African Princess leo hii amefanya uzinduzi wa kampuni na ofisi yake mpya ambayo inajikita kutoa huduma za sherehe, harusi pamoja na wahusika wake wote.

Advertisements

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Nandy ameonesha pia logo ambayo itatumika kuitambulisha kampuni hiyo pia, ameeleza kuwa amenunua frizer 200 kwa ajili ya biashara yake ya Nandy delivery na amekusudiwa kuzigawa kwa vijana jijini Dar es salaam.

Nandy akizungumza na waandishi wa habari picha Instagram
Advertisements

Aidha Nandy amesema kuwa amenunua mashine 70 ambazo atazifunga nyuma ya ofisi ya Nandy Bridal na zitatumika kudesign mavazi ya aina zote.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa anahesabu tukio hili kama hatua kwenye harakati za kimaisha, na analitaja kama moja ya ndoto ambayo leo hii imefanikiwa, pia mama mzazi wa Nandy ameeleza jinsi anavyofurahishwa na hatua aliyopiga mwanaye katika kazi zake.