Advertisements

Wanasayansi kutoka nchini Indonesia wametangaza kuwa wameweza kupata Mende mkubwa kabisa katika mlango wa bahari wa Sunda kati ya visiwa vya Java na Sumaria, kati ya mita 957 na 1,259 chini ya usawa wa bahari.

Mwaka huu taarifa za kisayansi zimekuwa zikihusisha mambo mengi ukilinganisha na miaka iliyopita hivi karibuni, ukianza na dunia ilipokabiliwa na janga la corona, nzige wanaokula mazao picha zilizopigwa kuonesha jua kwa ukaribu na hivi sasa mende mkubwa apatikana huko Sunda.

BOFYA KUSOMA ZAIDI…

Advertisements

Mende au Kombamwiko huyo ni jamii ya isopodi wenye uhusiano wa mbali na kaa na kamba ambao wako tambarare, miili yao ina ugumu mfano wa chawa anayeishi chini kabisa ya bahari

Kwa kawaida wadudu hao hukua mpaka kufikia ukubwa wa sentimita 33 na huchukuliwa kwamba ndio wakubwa zaidi, lakini kuna spishi nyingine ambayo ukubwa wao kuanzia kichwani hadi mkiani ni sentimita 50.

Msimamizi wa Utafiti huo kutoka taasisi ya Sayansi ya Indonesia, Conni Margaretha Sidabalok amesema kuwa “ukubwa wake ni wa juu zaidi”.

Kombamwiko au Mende huyo amepatikana katika mlango wa bahari wa Sunda Picha na BBC-Swahili
Advertisements

Kupitia jarida la Zookeys timu hiyo imeeleza kuwa kuna aina saba za pekee za spishi ya isopodi ambazo ni kubwa na zinajulikana duniani, pia ni mara ya kwanza Mende mkubwa namna hiyo anapatikana katika kina cha chini cha bahari ya Indonesia.

Kulingana na Makumbusho ya Kitaifa ya Viumbe asili ya Uingereza imetoa nadharia mbalimbali ambazo zinaelezea kwanini spishi zilizopo chini ya bahari huwa ni wakubwa sana.

Uhitaji wa Oksijeni ya kutosha ni moja kati ya dhana iliyotolewa ili kujibia nadharia hiyo, Wanyama wanaoishi chini ya kina cha bahari huwa wanahitaji oksijeni ya kutosha hivyo miili yao huwa ni mikubwa na miguu mirefu.

Dhana nyingine ni kwamba chini ya bahari wanyama wawindaji huwa ni kidogo hivyo jambo hili huwapa fursa ya kukua na kuwa wakubwa sana

Kombamwiko hao hula wanyama waliokufa chini ya bahari, Picha na BBC-Swahili
Advertisements

Hata hivyo Mende hawa huwa na nyama kidogo sana mwilini hivyo kuwafanya kutopendelewa na wanyama wawindaji, pia wana pembe ndefu na macho makubwa ambayo huwasaidia katika makazi yao yenye giza.

Aidha kwa mujibu wa Makumbusho ya Taifa ya Viumbe vya asili ya Uingereza inasema kuwa umeng’enyaji wao wa chakula huwa ni polepole sana, inasemekana kuwa mdudu jamii ya isipodi hii ambaye alikuwa ameshikiliwa Japan aliishi kwa miaka mitano bila kula chochote.

Chanzo BBC- Swahili