Advertisements

Mwanamitindo maarufu kutoka nchini Marekani Kimberly Kardashian maarufu kama Kim Kardashian amejitokeza hadharani na kuvunja ukimya kwa kuzungumzia matatizo ya afya ya akili ya mumewe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kim ameandika “Kama munavyofahamu Kanye ana tatizo la hisia zinazobadilika badilika yeyote mwenye tatizo hili au mpendwa wake anayepitia tatzio hili anajua vile linavyoweza kusunbua au machungu ya kuuelewa”

Advertisements

“Ni mtu mwerevu ambaye ni vigumu kumwelewa, wakati mwingine maneno yake hayaendani na nia yake” amesema Kim Kardashian.

Aidha katika ujumbe wake iku ya Jumatano Kim Kardashiana ambaye pia ni mashuhuri kwa uigizaji wa vipindi vya televisheni amesema kuwa “hajawahi kuzungumzia hadharani matatizo ya akili ya mume wake jinsi yanavyoathiri familia yake “kwasababu ninalinda sana watoto wangu, pia kuna haki ya faragha linapokuja suala la afya yake”

“Lakini leo naona nizungumze kwasababu ya unyanyapaa na dhana potofu kuhusu afya ya akili yake, wale wote wanaoelewa matatizo ya akili au hata tabia ya kulazimisha wanajua kuwa familia haina la kufanya labda mtu awe ahajafikisha umri wa kutambulika kama mtu mzima” ameongeza

Kanye West
Advertisements

Kim Kardashian ameeleza kuwa mume wake huwa anakosolewa kwasababu yeye ni mtu maarufu na wakati mwingine matendo yake yanaweza kusababisha maoni na hisia kali kutoka kwa mashabiki zake.

“Ni mwerevu sana lakini ni vigumu kumwelewa ambaye pia ni msanii na ni mtu mweusi ambaye amepoteza mama yake na anatakiwa kukabiliana na shinikizo la kutengwa ambako kumesababisha matatizo ya afya ya akili yake” aliongeza Kim

“Walio karibu na Kanye wanaelewa ni mtu wa aina gani, moyo wake na jinsi moyo wake ulivyo na wanaelewa kuwa wakati mwingine maneno yake ahayaendani na nia yake, japo kuishi na matatizo ya akili hakudidimizi ndoto wala ubunifu wake”

“Hii ni sehemu ya kipaji chake na kama ambavyo sisi sote tumeshuhudia ndoto zake nyingi zimetimia, naomba vyombo vya ahabri na umma watupe upendo unaohitajika ili tuweze kukabiliana na hili”.

Kanye West n mmoja kati ya wanamuziki wakongwe na maarufu sana nchini Marekani hivi sasa amekuwa akitrend kutokana na harakati zake za kutaka kuwania kiti cha Urais Marekani, japo hivi karibuni ameweka chapisho kupitia ukurasa wake wa twitter lililonesha kughairi kwa nia yake.

Mbali na kugombea urais msanii huyo anatarajia kuachia albamu yake muda wowote inayoitwa DONDA.

Kanye West na Kim Kardashian wameoana tangu mwaka 2014 na wamebarikiwa kupata watoto 4 kwa pamoja.

PICHA ZA KANYE WEST NA FAMILIA YA KARDASHIANS

Familia ya Kanye West siku ya Happy fathers day
Advertisements
Kim Kardashian akiwa na watoto wake picha Instagram
Advertisements
Advertisements
Kardashians picha Instagram
Advertisements
picha na Hollywoodlife.com