ANGALIZO Majina yote yaliyotumika katika chombezi hii ni majina ya kufikirika tu, hayajalenga kumtaja mtu yeyote.

“Camilla naomba unielewe natamani… natamani sana nikuoe hata leo hii nipo tayari”

“Jason najua unatamani kueleza upendo wako kwangu kwa vitendo, lakini angalia ni miezi sita tu tangu nikujue….” Camilla alijibu.

“Camilla miezi sita!! miezi sita ni mingi kumtambua mtu na tabia zake isitoshe mimi nimekufahamu wewe muda mrefu mno kabla hata hujanijua…tafadhali nakupenda Camilla” Jason alizidi kuchimbia msimamo wake.

“Jason kwanini unatamani kunioa mapema hivi?” Camilla aliuliza

“Camilla mpenzi wangu… maisha ni mafupi mno natamani nikae nawe angalia tayari nina nyumba nzuri nina magari lakini sina mke,..!! halafu pia nikikuoa nitakujengea heshima mpenzi wangu wewe hulioni hilo? Jason alieleza.

“Jason sawa nimekuelewa lakini.. laklni naomba basi muda kidogo nifikiri juu ya hili tafadhali mpenzi wangu..”

MIEZI SITA NYUMA

Kama ilivyo ada kwangu kila jumapili ikifika lazima niende kufanya ibada na hata zile siku za katikati huwa nahudhuria ibada za fellowship kwa sana tu, nilijiandaa tayari kulekea kanisani dereva wa bodaboda alikuja kunichukua na kunipeleka.

Nilifurahia mno ibada ya ile siku nilipenda mahubiri na nyimbo za kuabudu, kwani ndizo nyakati ambazo hunivuta mbele ya Mungu kwa haraka zaidi.

Tulipokuwa tukitoka nje nilimuona kijana ambaye ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona pale kanisani, ilikuwa rahisi kumtambua kuwa ni mpya kwani kanisa letu halikuwa na waumini wengi sana.

Nilishangazwa na jinsi alivyokuwa akiniangalia kwa makini sana, kila nilipojaribu kujichanganya miongoni mwa waumini wengine bado alikuwa akiniangalia kunifuatailia tu.

Alikuwa amevaa suti nyeupe ambazo zilimkaa vizuri sana, nilimuongalia kwa umakini nilimuona kaka kijana yule akienda kusimama upande wa wageni ambao wametoka kanisa tofauti na la kwetu kwani kila baada ya muda fulani huwa tunafanya ibada za kutembelea makanisa mengine.

Advertisements

Mchungaji wetu alimaliza ibada na kuturuhusu kuondoka kwa amani, nilitoa simu yangu ya mkononi ili kumpigia dereva wa bodaboda niliyemzoea aje kunifuata, ghafla nilihisi baridi begani kwangu nilipogeuka nyuma niliona sura ya yule mkaka ambaye alikuwa akiniangalia sana tukiwa ibadani.

Aliniita kwa jina na kunisalimia nilbaki nikimuangalia tu pasi na kujibu salamu zake nilibaki kama nimeopigwa na bumbuwazi hivi, moyoni mwangu niliogopa mno kwani nilianza kuhisi kama malaika wa kiume amesimama mbele yangu na zile suti nyeupe alizovaa.

Alinisalimia tena kwa mara nyingine na hapo sasa nikamsikia sawia kisha nikamjibu salama tu na kumuuliza ni kwa vipi ameweza kulijua jina langu wakati nina uhakika ni mara ya kwanza tunakutana.

Aliniambia kuwa jina langu amelisikia kutoka kwa mchungaji wangu aliponitolea mfano wakati wa mahubiri, alinieleza pia kuwa yeye anatokea kanisa jirani hapahapa Dar es salaam, nilimwambia nafahamu kwani tayari mchungaji alishawatambulisha.

Nilimuona akitaka kusema neno ila akaghairi kisha akaingia mfukoni mwake na kutoa kadi ambayo ilikuwa imeandika namba zake za simu pamoja na jina lake kamili, na kunipatia niliipokea kisha nikamwambia asante na kutoweka maeneo yale, sikutaka mazoea kabisa maana sikupenda kujikumbusha kumbusha yaliyonikuta huko nyuma.

Nilifika nyumbani Tabata Segerea ambako nilikuwa nikiishi katika nyumba ya kupanga niliiingia ndani na kujilaza kitandani kuanza safari ya kuutafuta usingizi kama ujuavyo wadada wa nyumba za kupanga tunavyojua kulala mchana.

Siku ile kila nilipojaribu sikuweza kupata hata lepe la usingizi, akilini mwangu ilijaa sura ya yule mkaka ambaye nimekutana nae kanisani, kila nilipotamani kutomuwaza bado nilibaki nikizidi kumuwaza tu, nilijiuliza maswali mengi ni nani yeye na anataka nini kwangu.

*********

Usiku ulipoingia ndipo niliona muda muafaka wa kuitazama tena ile kadi ambayo alinipatia kule kanisani, niliitoa katika mkoba wangu nilipoiangalia nilikuta imeandikwa jina la JASON DESMOND pamoja na namba za simu.

Nilivuta simu yangu ya mkononi huku presha taratibu ikianza kunipanda ili adhima yangu usiku ule ilikuwa ni kutaka kumtambua mtu huu ni nani na kipi alikuwa anataka kutoka kwangu.

Simu iliiita kwa muda kadhaa kisha ikapokelewa niliposikia sauti yake nikajitambulisha kuwa ni mimi Camilla wa kanisani, alionekana kama tayari ameshanijua kisha simu ikakatwa ghafla, kisha yeye akapiga tena.

Tuliongea mambo mengi sana na Jason alinieleza mahali anapoishi, kazi yake na nia yake kunitafuta mimizaidi ni jinsi alivyotamani kuniona tena kabla hata jumapili nyingine haijafika, binafsi sikuwahi kudhani kama Jason angekuwa ni kijana mcheshi kiasi kile alinieleza mambo mengi sana kuhusiana na yeye usiku ule.

Advertisements

Tangu hapo urafiki wangu na Jason ulianza kukua taratibu alionekana ni mtu aliyependa ucheshi sana, muda mwingi aliutumia kunipigia simu usiku kwani mchana aliniambia huwa anakuwa kazini.

Baada ya wiki kadhaa kupita Jason aliomba kupafahamu kwangu haikuwa rahisi sana kumkubalia aje kwangu lakini kwa kuwa niliona ni kijana niliyekutana naye kanisani niliamini asingeliweza kuwa mtu mbaya kwangu hivyo nilimuelekeza mpaka kwangu ninapoishi Tabata.

Mchana ule nikiwa nimekaa nje ya chumba changu niliona gari ya rangi ya kijivu aina ya JEEP ikisimama mbele ya ua wa nyumba yetu, nami nilijua tu kuwa ni Jason ndiye aliyekuwa anashuka ndani ya gari hiyo, niliinuka kwenda kumpokea mgeni wangu.

Alishuka ndani ya gari akiwa amevalia suti nyeusi nzuri, hakika zilimpendeza kweli kweli kwenye mwili wake, nilimkaribisha mpaka ndani kisha nikampatia kiti aweze kukaa.

Moyoni mwangu nilijisikia aibu kidogo wani Jason alionekana ni mtu mzuri sana, mtanashati na mwenye pesa na hadhi yake si ya kuingia kwenye kichumba kidogo kama changu tena chenye kitanda meza na kistuli kimoja tu pamoja na vyombo vyombo ndani. nilijihisi kama nina mkosi hivi.

Japo Jason alionekana kutokujali na hali aliyoikuta chumbani mwangu, bado akili yangu haikuweza kutulia, baada ya maongezi ya muda mchache nilimuomba Jason aniruhusu nimeletee chakula, naye akakubali.

Siku ile nilijitahidi kupiga chakula chenye hadhi kidogo tofauti na jinsi nilivyojizoesha nikiwa mwenyewe, nilimuandalia chakula kisha nikamkaribisha kwa ukarimu sana, nami nikamuomba nitoke nje ili nimuacha ale mana hivyo ndihyo nilivyokuwa nimefunzwa na wazazi wangu.

Jason alinishika mkono na kuniomba kusalia palepale kwani bado anatamani kuendelea mazungumzo na mimi, nilijaribu kuleta pingamizi katika lile ila mwishowe nilimkubalia tu.

Alikula chakula na alinishukuru baada ya kumaliza kisha akanieleza kuwa ameniletea zawadi alinikabidhi mfuko ambao alikuwa ameshuka nao kwenye gari nami nikamuomba kuufungua ili kuona nini ameniletea, hakika nilishangazwa na kile nilichokiona “gauni zuri jekundu”.

Nilimshukuru sana Jason kwa zawadi yake, nilichukua na kuiweka katika begi langu. huku nikimuangalia Jason ambaye alikuwa ameniita kwa jina langu wakati huo, nilitege sikio kwa makini kumsikiliza,…

Advertisements

“Camilla nina jambo sijui kama utalikubali…” Jason aliniambia

“Nieleze tu Jason kwanini nikatae nasi tumeshakuwa marafiki jamanii?..” Nilimjibu Jason huku nikijitetea kabisa

“Naomba siku ya jumapili baada ya kurudi kanisani nikupeleke mahali fulani tukafurahi kidogo..” Jason aliniambia

“Unamaanisha out!!… tutoke out?!!… mmh naogopa Jason tafadhali..” Nilimjibu kwa mshangao mno

“Tafadhali Camilla nakuomba… nitakurudisha nyumbani mapema sana wala sitakuchelewesha nakuahidi..” Jason aliendelea kusisitiza

Alinibembeleza juu ya ombi lake mwishowe nikaamua kukubali, japo moyoni mwangu nilikuwa na uoga lakini sikuwa na budi nilimkubalia.

Baada ya muda mfupi Jason aliaga na kuondoka huku akiwa ameniachia mtihani mkubwa sana, nilisimama nje ya ua wetu huku nikimsindikiza kwa macho, moyoni mwangu nilihisi kama bahati kupata rafiki wa kiume ambaye ana maisha mazuri na mtanashati kama Jason nilijisikia faraja sana.

JUMAPILI KANISANI

Siku huwa hazigandi hata uombe vipi labda enzi za mababu zetu, Jumapili ambayo niliahidiwa mtoko tayari ilishafika sikuwa na budi nilitinga nguo yangu mpya zawadi kutoka kwa Jason, kwani alisema kuwa atanipitia kutoka kanisani.

Advertisements

Nilipofika ibadani bado mawazo yangu yalikuwa kwa Jason na jinsi nitakavyoweza kukabiliana naye katika huo mtoko alioniomba, nilishiriki ibada japo si kama iwavyo siku zote baada ya ibada kuisha tu nilitoka nje.

Nilishangaa kuiona gari ya Jason tayari ipo katika sehemu ya kuegeshea magari, nikajisemea moyoni mwangu kuwa mmh huyu mtu hapotezi muda hata kidogo tu ooh!!… nilipoiangalia zaidi niliona gari yake ikiwasha taa za pembeni kama ikitoa ishara hivi nami ikabidi nijiongeze tu.

Nilianza kutembea kuelekea kule, nilipofika kwenye gari yake nilifungua mlango wa mbele na kuingia ndani, nilimuona Jason akiwa amevalia nguo nyeupe nzuri, kola za shati yake ikiwa imepambwa kwa rangi iliyofanana na dhahabu, nilimuangalia kwa umakini kama ndiyo mara ya kwanza namuona.

Moyoni mwangu nilijisemea huyu kaka anapenda kunichanganya changanya kwa mavazi yake mmh!! ona alivyopendeza mno amekuwa handsome boy la ukweli ooh!,hakika Jason alijua kuichota akili yangu barabara nguo alizovaa zilikuwa zinamatch sawia kabisa na nguo aliyonipa kama zawadi.

Alinisalimu akaniomba kufunga mkanda kisha safari ikaanza, gari ilitembea kama mwendo wa masaa matatu hivi kisha tukaingia mtaa ambao niliujua kuwa ni Mbezi Beach, ghafla gari ikasimama mbele ya geti moja kubwa sana lenye rangi nyeusi na kupiga honi.

Advertisements

Tuliingia ndani ya jumba lile gari ikaongoza mpaka sehemu nzuri ya kuegesha magari, niliposhuka sikuamini macho yangu nilihisi kama nimeletwa kwenye kasri ya kifalme, nyumba ya ghorofa kubwa nzuri iliyopambwa kwa kila rangi nzuri tena yenye kuvutia, nilibaki nimepigwa kwa bumbuwazi tu.

Jason alinishika mkono na kuniambia Camilla karibu nyumbani kwangu suiogope jisikie huru kwa chochote kile kwani sijaoa, sina mpenzi wala mtoto hapa nyumbani naishi na mfanyakzi tu kwahiyo usijali leo wewe ndo utakuwa mama humu ndani.

Nilifurahi kusikia hivyo japo moyo wangu uliogofya mno nikijiringanisha na kule nilikotoka duh!…. tulielekea mlango mkuu wa jumba lile nilimuona Jason akiweka dole gumba lake mlangoni kisha mlango unafunguka nikaguna tu mh! Jason..

“Yeeeh Camilla ni mlango unaofunguliwa kwa fingerprint… lakini pia ipo mingine inafunguliwa kwa kadi” Jason alijibu mguno wangu.

Nilipelekwa mpaka sebuleni kisha nikakaa na Jason huku akiniangalia na kutabasamu tu akaniambia nimsubiri aniletee kahawa ili kunituliza mana naonekana bado nina kapresha. Baada ya dakika chache alileta kahawa vikombe viwili kisha tukaanza kunywa panoja huku hadithi za hapa na pale zikiendelea.

Tulikaa pale nusu saa nzima huku tukipiga soga tu ghafla Jason alibadilika hali na kunifuata mpaka kwenye sofa ambalo nilikuwa nimekalia, nilianza kumuona Jason akama mtu aliyetaka ksuema jambo fulani lakini anashindwa aanzie wapi.

Alinishika mkono wangu wa kulia huku akiniangalia usoni pangu, macho yangu yalipogongana na yake sikuwa tena na uwezo wa kuvumilia nilitazama chini kwa aibu, aliniita Camilla…

Muda uo ilikuwa ni vigumu kuitikia jina langu, hasa nilipotambua kuwa nipo katika himaya yake na nisingeliweza kufanya jambo lolote lile, niliogopa asije akanitaka kimapenzi tu niliogopa sana

“Camilla… umekuwa rafiki mzuriii sana kwangu.. asante sana” Jason aliniambia

“Asante pia Jason nafahamu sisi ni marafiki tangu mwanzo na huu sasa ni mwezi wa tatu tu tupo katika urafiki wetu…” Nilimjibu Jason

Jason alinisogelea zaidi jambo ambalo lilinistua mno, alinikumbatia kisha akanieleza karibu na sikio langu

“Camilla natamani urafiki wetu uwe zaidi ya urafiki… ebu tazama tulivyostawi pamoja katika urafiki, itakuwaje endapo tutaongeza hisia zingine zaidi ya hizi?…” Jason aliniuliza.

“No, no Jason No pls tayari hisia za kirafiki zimeshastawi ndani yetu haipendezi kukuza jambo lingine tena…” Nilimjibu huku nikiwa nimeangalia chini.

“Ni kweli lakini nashindwaaa…!! ninateseka Camilla kila nionapo wavulana pale nyumabani kwenu nasikia wivu moyoni… nimevumilia nimeshindwa au una…”

“Hapana sina… lakini sihitaji tu kwa sasa natamani kuwa mwenyewe.. ” nilimkatiza Jason kabla hajamalizia sentensi yake.

Advertisements

Nilimuona Jason kwa mara ya kwanza akinipigia magoti huku sura yake ikionesha huruma tu, moyoni mwangu nilikuwa najiuliza huyu ni mkweli au ananiigizia tu hapa, hivi mimi mtu wa chini kabisa ataniweza kweli…

“Camilla ebu tizama ulivyo mrembo hakuna kifani, nimeona wengi sana hata uko ulaya nilikokuwa masomoni lakini bado moyo wangu umeuteka wewe…”

“Tafadhali Camilla!! nipe nafasi moyoni mwako nami nikuonyeshe upana wa bahari ya mapenzii… natamani nikuite hua wangu wa pekee” Jason alizidi kuniambia maneno yake ambayo yalinifanya nianze kutokwa na machozi ghafla…

“Jason pls kwanini lakini unanifanyia hivi… aaah… why Jason!!” Nilimuuliza Jason huku machozi yakinitoka

“Camilla nakuomba unipe nafasi nibadili maisha yako, ebu angalia jinsi itakavyopendeza ukiwa mama nami nikawa baba ebu angalia mawanda ya mapenzi yatakavyokuwa hayana kikomo tafadhali nipe nafasi Camilla….”

Chapisho lijalo tutapata kufahamu kipi Camilla aliamua kumjibu Jason… Je aliweza aliweza kutoka salama katika jumba la Jason… ?

Itaendelea…. Ingiza email yako hapa chini ili kujiunga nasi tutakuwa tukikutumia hadithi tamu kwa ajili yao