Advertisements

Wachezaji wanne nyota kutoka katika klabu ya Yanga wanasadikika kuwa hawatokuwepo jangwani katika msimu ujao kutokanana sababu mbalimbali ikiwemo zile zinazodaiwa kuwa ni uboreshaji wa kikosi.

Mpaka hivi sasa timu hiyo ambayo inanolewa na kocha mkuu Luc Eymael kutoka Ubelgiji inapambana kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili huku ikiwa imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FCkatika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

SOMA PIA;

  1. Yanga kushusha majembe mapya Jangwani
  2. Niyonzima aitia presha Yanga SC
  3. Yanga SC yamkata mshahara Morrison, Sababu na wito uliotolewa na klabu hiyo
  4. Memories of the Sea lady

Miongoi mwa wachezaji ambao wanataja kuondoka kikosini hapo ni pamoja nyota ambaye amecheka na nyavu mara 10 pamoja na pasi moja, David Molinga. Ikiwa anadaiwa kuwa ameshapata timu nyingine nje ya Tanzania.

Advertisements

Aidha nyota mkongwe kikosini hapo, Mrisho Ngassa ambaye inadaiwa kuwa tayari ameshapata ofa nchini Kenya pia dili lake klabuni hapo lipo mbioni kumalizika hivyo ana budi kusonga mbele zaidi.

Nyota wengine ni Andrew Vicent “Dante” pamoja na Tariq Seif mwenye mabao matatu pi wanatajwa kutokuwa kwenye hesabu za Eymael msimu ujao.

WordPress.com