Advertisements

Mwinyi Zahera, Kocha wa zamani wa Yanga azungumza lake la moyoni jinsi anayotamani mfungaji namba moja klabuni hapo David Molinga aendelee kubaki mpaka msimu ujao kwani bado kiwango chake kipo juu.

Zahera anamfananisha Molinga kama Meddie Kagere na John Bocco wa Simba wachezaji mahiri ambao wanacheka na nyavu muda wowote.

SOMA ZAIDI

Advertisements

Akizungumza jijini Dar es salaam Zahera amesema kuwa Molinga ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango cha juu klabuni hapo, ambaye anatakiwa kupewa nafasi ili aweze kufunga mabao zaidi kama vile Kagere wa Simba.

“Watu wengi walisema Molinga hafai huyu ni mchezaji mzuri na anaweza kuisadia Yanga, Kocha anatakiwa amuelewe Molinga ni mchezaji wa aina gani anacheza vipi, ufungaji wke hautoautiani na Kagere na Bocco” Zahera alisema.

“Nilisema atafunga mabao mengi akipewa nafasi atafanya vizuri zaidi, takwimu ya mchezaji ndiyo inayoonesha kama mchezaji ni mzuri au mbaya” Aliongeza.

Anatakiwa amjue ni mchezaji wa aina ani afanyishwe mazoezi ya kufika ndani ya boksi ili aweze kufunga mabao mengi, alikuwa anawekwa benchi hapati nafasi ya kucheza ndio maana alishindwa kuonyesha kiwango chake hapo nyuma” alimalizia Zahera.