Advertisements

Uongozi wa lebo ya WCB umeanika viingilio vilivyopangwa ambavyo watu watalipa ili kuingia kwenye usiku wa shukrani ya Zuchu utakaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City tarehe 18 July.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa lebo hiyo Naseeb Abdul alipokuwa akiongelea onyesho la msanii huyo.

Daimond Platnumz amesema kuwa onyesho hilo wanataka kulifanya kwa viwango vya kitofauti hivyo mpaka viingilio vimetofautiana kulingana na mahitaji ya watu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameweka chapisho lilionesha viwango vya kiinglio ambapo ameandika ” IAM ZUCHU asante nashukuru 18th July 2020 Mlimani City Hall siwezi kusubiri kabisa tiketi 50,000 kawaida, 100,000 VIP, Milioni 1 Table, Milioni 3 VIP table Milioni 5 VVIP Table na kuanzia kesho zitakuwa zinapatikana ofisi za Wasafi na maduka yote ya vunja bei”

Advertisements

Kwa upande wake msanii Zuchu amesema kuwa nusu ya mapato yatakayopatikana ameomba yaende kwa wasichana wenye uhitaji.

#Picha

Advertisements
Advertisements
Usiku wa Zuchu
Advertisements